Aaron Ally(Dj Aaron Tanzania)Mratibu wa‘All-stars Students Awards Akiongea Kwenye Kipindi cha Morning Trumpet kuelezea tuzo hizo.
Dj
wa zamani wa Clouds FM, Aaron, yeye na Team yake(Ms Chiku Lweno, Mwl.
Dany Mtanga) wameanzisha Tuzo walizoziita All-stars Students Awards.
Hizo ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari A-level na O-level za Afrika Mashariki.
Alhamisi hii Dj Aaron alialikwa kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha
Azam TV kuongelea tuzo hizo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam.
Aaron
amesema tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa
shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi
watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita. pia na
walimu husika ambao ni chachu ya wanafuzi ambao wamefanya vizuri kwenye
hayo masomo.
Tuzo hizo zitaaangalia namba moja wote waliongoza katika nchi zote za Africa Mashariki
Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili, Hesabu, Fizikia, Kemia,
Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo utaanza katikati ya mwezi wa
sita.pia Special Talents, Michezo na Shule bora
No comments:
Post a Comment