Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva akiongea na mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Luis Velarde wakati wa ziara ya waandishi hao katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Mtaalamu wa maabara katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga akiendelea na kazi ya kufanya vipimo vya malaria kwa kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) ambayo majibu yake hutolewa baada ya dakika 15.
Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari wamewasili Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe.
Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakimsikiliza Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja (hayupo pichani) walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Familia ya Salumu Rashidi wa kijiji cha Masatu kilichopo wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakiwa na mtoto wao Mohammedi Salimu ambaye ni miongoni mwa watoto waliopo kwenye mradi wa kudhibiti malaria wilayani huo. Kushoto ni mama yake Mohammedi Monica Mugunda.
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) wakitumbuiza wakati wa zaira ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani walipotembelea zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria. (Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Tanga)
No comments:
Post a Comment