Advertisements

Thursday, May 5, 2016

Wapenzi wa Jinsia moja wapinga ukaguzi wa 'tupu ya nyuma'

wapenzi wa jinsia moja

Wanaume wawili wanaosema kuwa maafisa wa polisi wa Kenya waliwalazimisha kufanyiwa ukaguzi wa tupu ya nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo kuwa ukiukaji wa katiba.
Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa ukaguzi wa magonjwa ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa kwao mnamo mwezi Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja.

Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria nchini Kenya na adhabu ya makosa hayo ni miaka 14 jela.

Mahakama ya Mombasa imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu.

Chini ya sheria ya kimataifa ,ukaguzi wa lazima katika tupu ya nyuma ni kitendo cha kikatili,unyama na ni sawa na mateso kulingana na kundi la haki za kibinaadamu Human Wrights Watch.

3 comments:

Anonymous said...

Kenya, kupokea misaada ni ok lakini msipoteze dignity yenu.Maana mnapoelekea siko..

Anonymous said...

Sasa kama jumuia ya kimataifa inasema ni ukatili,unyama na mateso kwa mume kufanyiwa ukaguzi wa lazima wa hiyo sehemu yao ya mwili isiopata jua kwanini jumuia hiyohiyo iridhie na kuhalalisha wanamume kuchezeana huko nyuma? jamani hatuoni kuwa hii ni double standard? Ni maoni yangu binafsi tu na vile vile sifikirii kama kuna ukaguzi wa hiyari kutokana ualisia wa neno ukaguzi.

Anonymous said...

Mbona mashoga ama wasnge wapo siku zote nchini na tunalifahamu hili. inakuwaje leo tunajifanya kushangaa. hebu tuwe wa kweli.

ni kweli hatujakubali uwazi huo lakini waacheni ili mradi hawakushurutishi