Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametaka watuhumiwa waliombaka mwanamke eneo la Dakawa mkoani Morogoro na video yake kusambazwa wafikishwe mahakamani haraka.
Haya ndio maneno ya Waziri Ummy Mwalimu katika Akaunti yake ya Facebook:
Ndugu zangu! Nimeiona dakika chache zilizopita video ya mwanamke akidhalilishwa na wanaume wawili (mashuka yanaonyesha eneo la Tiff Lodge Wami - Dakawa). Nakemea kwa nguvu zangu zote waliofanya kitendo hiki. Ni unyama uliopitiliza. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu. Hatuwezi kuuvumilia.
Nimeshamuomba Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP wachukue hatua stahiki haraka.
Pia nawaomba sana ndugu zangu msisambaze hizo video. Hiyo ni kuendelea kumdhalilisha huyo dada. Amebakwa na pia wamerekodi hilo tukio! Hii haistahimiliki na haivumiliki. Wanawake wote na wanaume wapenda haki na maendeleo ya wanawake tukemee kwa nguvu zetu zote unyama huu.
SOMA MAELEZO YA MDADA ALIYELETEWA VIDEO HIYO
Jana usiku kaka yangu mmoja kaniletea video iliyonifanya nisipate usingizi. Ni clip mbili za dada mmoja aliyetekwa na kuwekwa chumbani na wanaume wawili. Wamempiga picha za uchi na kumtendea tukio baya kabisa.
Yule dada analia na anajaribu kuficha sura lakini anapigwa na kuingiliwa kwa nguvu. Wanazungumza kiswahili. Wanaonesha ubakaji kwa kurekodi. Shuka la nyumba linasomeka Teth Lodge, ya BOX 63. Mahali ilipo hapaonekani vema lakini ni kama vile Wami Dakawa.
Sidhani kama huyu dada ataendelea kuishi kama binadamu wa kawaida maana kisaikolojia lazima atakuwa kaumia sana hata akibaini hii clip inasambazwa tayari. Nimeshindwa kuiweka hapa kwa kuwa inasikitisha sana. Naandika nikilengwa machozi.
Sihukumu, Mungu anisamehe lakini nadhani hawa wabakaji wanastahili adhabu kali kuliko zote tuzijuazo. Mungu ampe nguvu huyu binti
CHANZO: JAMII FORUM
No comments:
Post a Comment