Advertisements

Wednesday, May 25, 2016

YANGA YAITANDIKA AZAM 3-1 NA KUKUSANYA MATAJI YOTE JANGWANI HII NDIYO YANGA YA MANJI.


Yanga imefanikiwa kutwaa ndoo zote msimu huu zinazosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) baada ya kuichapa Azam FC kwa bao 3-1 kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA (Azam Sports Federation Cup) mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.
Washabiki wa Yanga kama kawa kama dawa tawi la whatsapp family 
Warembo wakiwa wabeba kombe.
Kushoto Ramadhani Hassan Kessy kulia Juma Mahadhi. . . Starring Jerry Murro.

YANGA SC imehitimisha msimu wa 2015/2016 kwa kutwaa mataji yote ya nyumbani, baada ya kuifunga Azam FC mabao 3-1 na kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, sasa Yanga ni mbabe asiyepingika wa soka ya Tanzania, baada ya awali kutwaa Ngao ya Jamii Agosti 22, mwaka jana waliposhinda kwa penalti 8-7 dhidi ya Azam FC pia baada ya sare ya 0-0 na mapema mwezi huu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na Israel Nkongo, hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji kutoka Burundi, Amissi Joselyn Tambwe dakika ya tisa kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.YANGA DAIMA 

No comments: