ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 19, 2016

YANGA YATINGA HATUA YA MAKUNDI AFRIKA MICHUANO YA CAF

Klabu ya Yanga jana ilifungwa bao 1-0 na wenyeji Sagrada Esperanca katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania hatua ya kufuzu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika katika uwanja wa Esperanca mjini Dundo, Angola.

Lakini Yanga wamefuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam, mabao ya Simon Msuva na Matheo Anthony.

Yanga inatinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho michuano ya CAF kwa mara ya pili tangu walipofanikiwa kufanya hivyo kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1998.

Timu hiyo Yanga wanatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho mchana wakitokea Angola

No comments: