Wednesday, June 8, 2016

ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI KUPITIA MTANDAO WA KIJAMII AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3 JELA AU KULIPA FAINI YA SH. MILIONI 7

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Wa Arusha,imemhukumu  Isack Habakuki(40) mkazi Wa Olasiti, kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni 7 kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli kupitia mtandao wa facebook.

Mshtakiwa amekiri kutenda kosa hilo na amekubali kulipa faini ambapo mahakama imeamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili. Katika awamu ya kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi kilichobaki cha sh mil 3.5.



Isack anayeishi Kata ya Olasite, anadaiwa kutoa lugha ya matusi na dhihaka kwa Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na alikamatwa Machi 23, mwaka huu mjini Arusha na kupelekwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kisha alirejeshwa tena Arusha Aprili 14, mwaka huu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.


Mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile,  Wakili wa Serikali, Gaudensia Massanja, alidai kuwa Isack alikuwa akikabiliwa na kosa moja ambapo kwa kufahamu na kwa makusudi mtuhumiwa huyo alitumia mtandao wa Facebook kwa nia ya kumtukana Magufuli.

Alidai kwamba mtuhumiwa katika ukurasa wake wa Facebook alichangia maneno yanayosema: “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana.”

7 comments:

Anonymous said...

DIASPORA TUMCHANGIE KUSEND MSG KWA SERIKALI

anonymous said...

Hivi bongo hakuna freedom of speech?

Anonymous said...

You can't compare American or western freedom of speech with African or Tanzanian one that is for sure a total madness. Forget about politics,we as Africans tend to respect our elders for the way we talk or treat them. This punk who as some people here have complaining that his right of freedom of speech has been violated, can he real call his own father bwege? As Tanzanian can you real call your own fathers mabwege? Magufuli is rather and husband apart from his political life so what kind of freedom of speech this guy is trying to send to the Magufuli family?

Anonymous said...

Hakuna freedom isiyokuwa na mipaka. Kutukana watu wengine hakuwezi kuwa sehemu ya freedom of speech! Kwa hili, kipimo cha uadilifu ni hiki: kama angemuita baba yake "bwege" ingekubalika na jamii yetu kama freedom of speech?

Anonymous said...

Bongo majanga kweli kweli,so sad,wacha sie tuendelee na kubeba mabox yetu ungaibuni kwa raha zetu,na freedoms of speech zetu,viongozi wa Tanzania mnanyanyasa sana raia,that's not fair,ukishakuwa kiongozi you have to be prepare na kashfa kibao,Obama kashatukanwa mara ngapi kwani amekufa???

Anonymous said...

Kuna watu wamekalia freedom of speech hakuna TZ Lahasha!Tusipotoshe vizazi vyetu kwa maadili yasiyo yetu,we still need Respect and Dignity.

chempro said...

Demokrasia za Kiafrika bado zinakua