Friday, June 3, 2016

Daktari: Diamond Anamuua Baba’ke!

Baba mzazi wa Diamond, Mzee Abdul Juma.

Mwandishi wa, Amani

DAR ES SALAAM: “Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa duniani linalotokana na kusheheni kwa mawazo ya kila wakati, husasan kuhusu maisha au afya. Kwa hiyo anachofanya Diamond kwa baba yake ni sawa na kumuua kwa sababu ya kumsababishia msongo,” ndivyo alivyosema daktari Rweyemamu wa hospitali moja ya jijini Dar.
Daktari Rweyemamu alizungumza na Amani hivi karibuni kufuatia habari zinazoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba amemtelekeza baba yake, Abdul Juma.

Msanii Diamond Platinumz

AZUNGUMZIA HISTORIA

“Nimekuwa nikisoma habari mbalimbali kwenye Magazeti Pendwa ya Global, lakini hili la Diamond kumtelekeza baba yake mimi naona lina mapana yake. Najua utetezi wa Diamond ni kwamba, baba alimtelekeza mama yake (Sanura Kasim) yeye akiwa mtoto.

“Kwa hiyo malezi yote, ameyapata kwa mama mpaka kufika kwenye kiwango cha mafanikio. Lakini pia nimewahi kusoma kwamba, baba aliomba msamaha yaishe, atambulike kama baba lakini mtoto akagoma.”

MAGONJWA YA BABA

“Kuna wakati nikasoma kwamba, yule mzee anasumbuliwa na miguu, mara sijui ugonjwa wa kansa ya ngozi. Pia amekuwa mtu wa kuumwa mara kwa mara.”

MSONGO WA MAWAZO

NI CHANZO 

“Yule mzee atakuwa na magonjwa mengi, hasa yanayotokana na msongo wa mawazo. Mawazo yake kwa sasa ni kitendo cha kuona mafanikio ya mwanaye akilinganisha na maisha yake magumu bila msaada.

“Binadamu yeyote, anapomwona mtu wake wa karibu amefanikiwa na yeye hali duni lakini huyo aliyefanikiwa anaweza kumsaidia yeye akaondokana na hali duni, lazima asumbuliwe na msongo.”

MIGOGORO, UGUMU

WA MAISHA

“Lakini pia migogoro inayotokea katika familia, ni moja kati ya sababu zinazoweza kumpa mtu msongo wa mawazo, hasa pale ambapo utaichukulia ‘serious’ kwa kuwa inagusa moja kwa moja maisha yake. Ugumu wa maisha unachangia pia.”

MWILI UNAVYOATHIRIWA

NA MSONGO

“Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo. Mwili unavyokutana na hali tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya muda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na jambo usilolitegemea, basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia kitu hicho.

“Mapigo ya moyo huongezeka, mapafu huchukua kiwango kikubwa cha hewa na mzunguko wa damu pia huongezeka na baadhi ya sehemu za kinga huzidiwa na mzigo mkubwa hivyo kutoa nafasi kwa viumbe adui kuushambulia mwili kirahisi.

“Msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa siku hadi siku ndipo kinga ya mwili inavyozidi kushindwa kubaini uwepo wa kichocheo cha cortisol, msongo unapunguza makali ya kinga ya mwili, hivyo matatizo ya afya huongezeka.”

UTAFITI

“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na World Health Organization, Shirika la Afya Duniani ‘WHO’, maradhi ya moyo, akili, ugumba, ukosefu wa nguvu za kiume na vidonda vya tumbo, pia yanacha-ngiwa na msongo wa mawazo.”

LAZIMA BABA

DIAMOND AWE HIVI

Kwa mujibu wa daktari huyo, lazima baba Diamond wa sasa atakuwa amebadilika tabia, kwamba atakuwa mpole na siyo mwenye furaha kwa muda mwingi.

“Kuishi kwa kubangaiza pesa za kula huku akiwa anajua mwanaye anazo, tena mpaka zinamzidia, baba Diamond atakuwa anamalizika polepole. Lazima kila akiamka, anasema; ‘mateso yote haya, mwanangu yupo lakini hataki kunisaidia.”

WITO WAKE KWA DIAMOND

Daktari huyo alisema kuwa, anamtaka Diamond kurejesha moyo wake nyuma, amtunze baba yake ili amuokoe na kumalizika.

“Namtaka Diamond ajue kuwa, anachomfanyia baba yake ni kumuua bila yeye kujua. Ukuta anaomuwekea katika usaidizi unamfanya mzee huyo kunyemelewa na magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo ambavyo kwa mazingira ya maisha yake yanaweza kumsumbua kwani yanahitaji kipato kizuri.
CREDIT:GPL

5 comments:

Anonymous said...

Ya Ngoswe mwachieni Ngoswe mwenyewe. Mbona mnamng'ang'ania Diamond? Ya kwake yanawahusu nini? Huyu Daktari au Mbabaishaji. Anatoaje ushauri kwa kusoma kwenye magazeti ya udaku? mambo ya familia yanakuwaga complicated sana. Watu wa nje mtasema tu. Waachieni wenyewe. Huyo baba Diamond mbona kila siku magazetini? angekuwa na busara asingetangaza mambo ya ndani. Na kuomba msamaha sio lazima kusamehewa.Baba akatae mtoto, ale maisha, akichoka alazimishe msamaha.
Muacheni Diamond na maisha yake hakuna msamaha wa lazima. Angekuwa hana shida huyo baba angeomba msamaha? alikuwa wapi kabla Diamond hajafanikiwa?

Anonymous said...

Je Diamond asinge kuwa na pesa baba yake angemtambua mwanawe?. Baba wengine hawana mana.kila siku huyu babu yupo kwenye ma blog. Tulia kama anakuta,atakufuata.

Anonymous said...

What goes round comes around....huyu mzee kama alimtelekeza mwanaye anamtaka wa nini akiwa na pesa zake.mimi ninavyo ona diamond hana makosa....nifundisho kwa baba wengine wanao telekeza wanao

Anonymous said...

Family dynamics ni ngumu sana kwa mtoto kuzidadavua kwa usahihi na kuweza kuegemea upande fulani. Mtoto unapaswa kuwa neutral kadri iwezekanavyo. Hukumu aliyoitoa Diamond ni sawa na hukumu ya kesi iliyosikilizwa upande mmoja; lazima iwe na chembechembe za biases!

Tumeshuhudia baadhi ya wamama wakifanya kila hujuma kuangamiza kabisa mahusiano ya baba na wanae, kwa sababu tu yeye haelewani na mwenzi wake.

Anonymous said...

Huyo ni daktari au mganga wa kienyeji??? Kivipi anamuua baba yake? Duniani huku kuna stress ila usipoweza ku-control stress mwenyewe hilo ni shauri lake na si wala la Diamond. Hao ni wale wazee wa Kiswahili ambao badala ya kusaidia watoto wao wafanikiwe kimaisha kwa kuwapa elimu na miongozo mizuri wanasubiri watoto wafanikiwe halafu wawatafute wakiwa na mafanikio japo kidogo ili wale kile watoto wao walichotengeneza.....yaani ni wazee tegemezi (kuanzia asubuhi hadi jioni wapo wanacheza bao)halafu wakiona watoto wao hawawagawii mali yao nusu kwa nusu wanaanza maneno na kuomba kuonewa huruma. Achaneni na magazeti hayo ya Shigongo yanayoandika habari za kuuza. Wewe mzee baba yake Diamond Platnumz unatakiwa ufanye kazi au kama ulifanya kazi ukiwa kijana kadai pension yako siyo kuomba kuonewa huruma huruma kwa watu.Ungekuwa baba yangu nisingekusikiliza kabisa angalau Diamond anakupa attention kidogo. Kama ulikuwa unafanya kazi ipo wapi akiba uliyoiweka?