Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limepokea malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu Uchaguzi
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Kinondoni (KIFA) uliofanyika Juni
12, 2016 kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar
es Salaam.
Kutokana na malalamiko hayo, TFF
imewaita wagombea wote wa ngazi ya juu wa KIFA wakiwamo viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo kuhudhuria kikao cha Kamati ya
Uchaguzi ya shirikisho kitakachofanyika kesho Jumamosi Juni 18, 2016
saa 3.00 asubuhi.
Pia, imewaita viongozi wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sambamba na Kamati za
Uchaguzi za DRFA kadhalika ile ya KIFA ambazo zilisimamia uchaguzi
huo ambao ulifanyika kwa mara ya pili mwishoni mwa wiki baada ya ule
wa kwanza kuahirishwa mwezi uliopita.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA
TANZANIA
1 comment:
Great news
Post a Comment