Sunday, June 12, 2016

MAALIM SEIF KUNGURUMA MAREKANI

Unguja. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amewaambia wafuasi wao kwamba wataendelea kudai alichodai ni ushindi wa chama chao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Maalim Seif aliondoka nchini jana kwenda Marekani na kesho atazungumzia kilichojiri kwenye Uchaguzi Mkuu na kusababisha chama chake kususia uchaguzi wa marudio wa Rais wa Zanzibar ulioipa CCM ushindi.
Mwanasiasa huyo anatarajiwa kutoa mhadhara katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Elimu ya Kimkakati na Kimataifa cha Marekani (CSIS) na utafanyika makao makuu ya taasisi hiyo mjini Washington DC kuanzia saa nne asubuhi.

1 comment:

Anonymous said...

Wangemsaidia kwa kumpatia matibabu badala ya kuigawa nchi