ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 21, 2016

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA MAFUNZO YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiriamali  yalioandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani, Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mhe. Mama Anna Mkapa akihutubia kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ambapo mgeni Rasmi wa ufunguzi huo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Ndugu Steven Martin akielezea kwa ufupi mafanikio ya mafunzo ambayo yametimiza miaka 19.

 Sehemu ya wakina ama waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani,Dar Es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Esther Mkwizu akizungumza na wajumbe walihudhuria mara baada ya unfunguzi rasmi wa mafunzo kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janetth Magufuli ,Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema wakifurahia jambo wakati wa shughuli za ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali wanawake ,kushoto ni Mwenyekiti wa wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
 Baadhi ya wakina Mama waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hotuba za  ufunguzi wa mafunzo ya wanawake wajasiriamali.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Jacline Maleko akisalimiana na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Wanawake Wajasiriamali yaliofanyika kwenye Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amehimiza wanawake wajasiriamali wa Tanzania Bara na Visiwani kujiunga na majukwaa ya kuwezesha wanawake kiuchumi yatakayoanzishwa kote nchini kwa ajili ya kupata elimu ya ujasiriamali.

Mheshimiwa Samia alitoa rai hiyo leo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) katika Bwalo la JKT Mgulani, Dar es salaam.

Alisema kama wanawake watayatumia majukwaa hayo ya kiuchumi  watakuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa bora, kutafuta masoko, kupanga bei nzuri za bidhaa na kupata fursa za mikopo.

Aidha, Makamu wa Rais aliwasihi wanawake wajasiriamali kuichukulia ajira hiyo kama ajira yo yote rasmi kwa kuwa serikali itaweza tu kutimiza azma yake ya kupunguza ukosefu wa ajira kupitia sekta ya viwanda vidogo vidogo ambavyo vingi vinaendeshwa na wajasiriamali.

“Kupitia majukwaa niliyoyataja ya kumwezesha mwanamke kiuchumi nitajihidi kuhakikisha kuwa majukwaa haya yanatoa majibu ya changamoto zinazowakabili wanawake wajasiriamli na kuchangia ukuaji wa ajira, kuondoa umaskini na kuwezesha ujenzi wa Taifa la viwanda,” alisema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa EOTF Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa alisema tangu Mfuko huo uanzishwe miaka 19 iliyopita umetoa mafunzo kwa zaidi ya wanawake wajasiriamali 30,000 na umewezesha wajasiriamali 14,500 kushiriki maonesho ya sabasaba ili kutangaza na kuuza bidhaa zao.

“Wanawake hawa wamejenga nyumba bora, kusomesha watoto, kulipia huduma za matibabu, shughuli za kifamilia kutokana na mafanikio ya biashara zao zilizoborehwa na mafunzo hayo.  

Mama Mkapa alimwahidi Makamu wa Rais kuwa mfuko huo utaendelea na jitihada zake za kutoa elimu kwa wanawake wajasiriamali na kuwawezesha kushiriki katika maonesho ya biashara.

Katika mafunzo hayo wanawake wajasiriamali wataelimishwa jinsi ya kupata mitaji na matumizi ya mashine za EFD; magonjwa hatarishi kama vile ukimwi, saratani na malaria pamoja na suala zima la mirathi na ujasiriamali kwa ujumla.

No comments: