Rais wa TFF Jamal Malinzi amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na vurugu zilizotokea katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Yanga na TP Mazembe ambapo mashabiki walifanya vurugu hali iliyopelekea jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Malinzi amesema wamechukua jukumu hilo kwa kuwa katiba inaruhusu kufanya hivyo lengo likiwa ni kuzuia athari zozote zinazoweza kujitokeza.
Aidha, Rais huyo amesema bado wanasubiri taarifa kutoka CAF juu ya vurugu zilizotokea nje ya uwanja muda mchache kabla ya mchezo huo kufanyika huku akisema Yanga wasubiri kudra za Mwenyezi Mungu ili kuepuka adhabu kutoka shirikisho hilo la soka Afrika.
Hata hivyo Malinzi amesema Yanga bado ina nafasi ya kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo kutokana na namna kundi lao lilivyo hadi sasa hivyo wao kama shirikisho wanawatakia kila la kheri katika maandalizi yao.
No comments:
Post a Comment