Mwanafunzi wa Madrasa AL-Mustakima Rashid Kimweli akisoma Quaran katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quaran yaliyofanyika mbagala bucha, jijini Dar es salaam wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran yaliandaliwa na Madrasa ya AL-Mustakima iliyopo Mbagala Bucha jijini Dar es salaam ambapo watoto wa kiislamu takribani 10 wenye umri kati ya miaka sita hadi 13 wa madrasa nne za Madrasa Tul – Mustakima ya Yombo Dovya, Mbagala Bucha, Madrassa Tul- ukutani na madrassa Tul Ismailia ya mtoni kijichi.
Mwanafunzi wa madrasa AL-Mustakima Zahra Mohamedi akipokea zawadi shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini katika kitabu cha Quaran.
Mwalimu mkuu wa Madrasa AL- Mustakima Ustaadhi Hassani Seleiman akimtunza fedha ustaadh Iddrisa wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran yaliyoandaliwa na Madrasa AL mustakima ya Mbagala bucha jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi wa madrasa AL-Mustakima akipokea zawadi shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini katika kitabu cha Quaran. ( Picha na Tamimu Adam).
Na Tamimu Adam
Wazazi na walezi wa kiislamu wametakiwa kuenzi na kuihifadhi Quran tukufu na kuipa heshima ya aina yake kwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki katika mashindano ya kusoma na kuifadhi Quran ili kuwawezesha kufahamu vizuri uislamu na kuwa muongozo katika maisha yao ya kila siku hapa dunia na kesho ahera.
Hayo yalisemwa na Ustaadhi Iddrisa kutoka Kigoma wakati wa mashindano ya kusoma na kuifadhi qurani yaliandaliwa na Madrasa ya AL-Mustakima iliyopo mbagala bucha jijini, Dar es salaam ambapo watoto wa kiislamu takribani kumi (10) wenye umri kati ya miaka sa sita hadi kumi na tatu wa madrasa nne ambavyo ni Madrasa Tul – Mustakima ya yombo dovya na mbagala bucha, madrassa Tul- ukutani na madrassa Tul Ismailia ya mtoni kijichi.
Naye Mwalimu mkuu wa Madrasa ya AL- mustakima ambayo ndio mratibu wa mashindano hayo Ustaadhi Hassani Suleimani alisema mashindano hayo yalishirikisha wanafunzi kumi ambao waligawanywa katika makundi makuu mawili kundi la kwanza ni wanafunzi watano kutoka vyuo vyote nne ambao walisoma na kuifadhi juzuu mbili na kundi la pili ni kwa wanafunzi ambao walisoma na kuifadhi juzuu tano.
Aidha , aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuwafundisha vijana kusoma na kuhifadhi kitabu cha mwenyezi mungu, kuipenda qurani na kuitumia katika maisha yao yote pamoja na kuwafundisha maadili ya kiislamu na maamurisho yake yote kwa waislamu. Aliongeza kuwa mashindano hayo yalisimamiwa na majaji watatu kutoka mbande ambao kwa ujumla walikuwa wanaangalia vigezo mbalimbali ikiwemo namna ya kusoma na kutamka maneno ya quaran kwa usahihi.
Kwa upande wake Imamu wa Msikiti wa mbagala charambe Sheikh Adam Mikidadi ambaye alikuwa miongoni mwa majaji wa mashindano hayo alisema kuwa mashindano yalienda vizuri ambapo yalifanyika kwa kiwango kilichotarajiwa, washiriki walisoma na kutamka quarani vizuri kabisa na kuweza kufikia vigezo vya mashindano kwa asilimia 85.
Sheikh aliwataka washiriki wote kuongeza bidii mwakani ili waweze kufikia asilimia 100 na kuwa mahiri katika kusoma, kuhifadhi na kukuza uislamu ndani ya jamii.
Pia aliwataka wazazi na walezi kuhamasika na kuisoma quaran tukufu ili iwe muongozo wao katika maisha yao yote na kwa wale wenye uwezo wawe na tabia ya kujitolewa kudhamini mashindano ya kusoma na kuhifadhi kitabu cha mwenye mungu.
Washiriki wa mashindano hayo walipewa zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza Zahara Mohamed alizawadiwa shilingi laki moja na thelathini kwa kusoma na kuhifadhi juzuu 5 kati ya juzuu thelathini na wa pili alizawadiwa fedha taslimu elfu themanini, tano na watatu alizawadiwa shilingi elfu sitini na tano na wengine walipewa elfu arobaini.
No comments:
Post a Comment