ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 27, 2016

MCHEZAJI BORA WA UMMISETA MUSA SAID KUONDOKA JUNE 29, 2016 KWENDA NCHINI UFARANSA

 Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, akizungumza na waandishi wa habari kuwaelezea juu ya safari ya mchezaji Musa Said anayetarajia kuondoka Jumatano ya Juni 29, 2016 kwenda nchini Ufaransa kwenye kambi ya kimataifa ya Copa Coca-Cola. Pembeni ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, Mchezaji Musa Said Bakari na Mwalimu wake wa Kibasila. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Na Devotha Kiwelo.
 MCHEZAJI bora wa mashindano ya UMMISETA yaliyofanyika mwaka jana mkoani Mwanza, Said Musa Jumatano ya Juni 29, 2016 kuelekea Ufaransa katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca - Cola ambayo imeandaliwa na kampuni ya kinywaji cha Coca - Cola .

Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alisema udhamini wa kampuni ya Coca - Cola imetambua umuhimu wa michezo hivyo kukubali kudhamini michezo kupitia shule za sekondari ili kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi ambao wanamalengo makubwa katika kuitumikia nchini yao kupitia michezo.

“Kwetu sisi imekuwa faraja kwa kuibua kipaji kichanga ambacho kitakuwa ni mfano wa kuigwa kama ilivyo kwa Samatta ambaye amekuwa kioo kwa jamii ya wanamichezo na hivyo kuomba makampuni mengine kujitokeza kwa ajili ya kusaidiana na Coca - Cola”, alisema.

Kiganja alimtaka Musa kuzingatia nidhamu kipindi chote atakachokuwepo kwenye kambi ili kujijengea heshima katika kukuza kipaji chake kwa kipindi chote ambacho atakuwa chini ya walimu wageni ambao hajawahi kukutana nao na hiyo italeta heshima nchini.

Kwa upande wa Meneja msaidizi wa chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, alisema wamefurahi kupata nafasi ya kudhamini mashindano hayo kwa kuwa ndiyo mara yao ya kwanza na imefanikiwa kufikia malengo ya kupata mchezaji ambaye atakuwa muwakilishi wa Tanzania katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca - Cola iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa.

Alisema Musa ataondoka kwa kupitia Nairobi kwa kuwa kozi inaanza kesho na kumalizika Julai 4, hivyo aliwataka wanafunzi wengine kujituma ili kufikia malengo kama aliyofikia Mussa.

“Sisi kama kampuni imekuwa ni faraja kwani tutakuwa tumeitangaza nchini kwa kupitia Mussa na hii itakuwa ni muendelezo katika michezo inayoendelea,”alisema.

Mussa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila ambaye alizaliwa Agosti 11, 2000 huku akiwa ni mchezaji tegemeo katika timu ya shule na Mkoa wa Temeke ambapo walitumia jina hilo kwa kupitia michezo.

No comments: