Sunday, June 12, 2016

MISA YA KISWAHILI - NEW YORK

Wakristu wapendwa,
Tumsifu Yesu Kristu.
Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi, wanapenda kuwatangazia ya kuwa,
Misa yetu ya kiswahili itafanyika Jumapili hii, tarehe 12 Mwezi Juni, 2016, Saa 8:00 mchana (Sunday 12, June 2016 at 2 pm). Tungeomba wakristu wote watanzania na Afrika ya Mashariki wajiunge nasi katika Misa hii. Na siku ya akina baba.
Tunawakaribisha watu wote wanaopenda kuhudhuria ibada ya Kiswahili.

Anwani yetu ni: Kanisa la Mt. Cecilia, 
120 East 106 Street, 
New York, NY 10029. 
Between Lexington and Park Avenue. 

Chukua Train # 6. Mpaka kituo cha 110 St. Halafu tembea ukirudi mpaka 106 St.

Ni matumaini yetu kwamba mtafika kwa wingi. Karibuni tumtukuze Muumba Wetu kwa lugha yetu ya Kiswahili.
Mbarikiwe. Kutoka kwa Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi

Karibuni...

2 comments:

mboya said...

kazi nzuri

jomki said...

Kiswahili daima kitukuzwe