Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na mara baada ya kufika ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma mwishoni mwa wiki na kuendesha semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) akisamiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili ofisini kwa Naibu Spika Bungeni mjini Dodoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo(UNDP) Alvaro Rodriguez amesema anaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa,kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato .
Akizungumza katika semina ya fupi wabunge kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa mwaka 2015 -2030 alisema, hakuna nchi ambayo inaendelea bila kufanya kazi hivyo shirika hilo linategemea kasi iliyoanza nayo Serikali ya awamu ya tano itaendelea ili kuleta maendeleo.
"Nimekuwa nikiona kazi zinavyofanya na serikali hii nimeridhika katika kupambana na rushwa,kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa umma pamoja kufanya juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya kodi, nimeridhika na jitihada za Serikali hii,"alisema Rodriguez.
Alisema anategemea kasi hiyo itaendelea ili kuweza kufanikisha malengo yaliyowekwa.
Alisema Malengo 17 ya Dunia ya Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na mambo mengine yamelenga kutokomeza umaskini, kuondoa njaa, usawa wa kijinsia na kuondoa utofauti wa kipato.
Rodriguez aliwasisitiza wabunge kuwa mabalozi wa kusimamia utekelezaji wa malengo hayo nchini na kuyafikisha kwa wananchi.
Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Paul Kessy alisema Tanzania imeshiriki kwa kiasi kikubwa katika maandalizi na kuathiri maudhui ya Malengo Endelevu ya Dunia kwa maslahi mapana ya Taifa na wananchi kwa ujumla.
"Hii ni pamoja na kuhakikisha baadhi masuala ambayo hayakukamilika katika utekelezaji wa ajenda ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) kama vile kupunguza umaskini, upatikanai wa ajira na kukuza uwezo wa nchi maskini hususani maendeleo ya teknolojia yanazinagatiwa vilivyo katika agenda mpya,"alisema Kessy.
Awali akifungua semina hiyo Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson alisema kazi ya wabunge ni kuangalia,kujadili na kupitisha mipango ya serikali hivyo wana jukumu la kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo endelevu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ( kulia) sehemu ya taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma mwishoni mwa wiki.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wabunge wakati wa ufungunzi wa Semina kwa wabunge kuhusu Malengo ya dunia ya Maendeleo Endelevu iliyoandaliwa na Umoja huo mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Mbunge akikubali hoja kwa kugonga meza wakati wa semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Paul Kessy akizungumzia utekezaji wa SDGs ambapo alisema uwe ndani ya mipango ya nchi wakati wa semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Mtaalam wa Masuala ya Uchumi kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP), Rogers Dhliwayo akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuyafikia Malengo Mapya 17 ya Maendeleo Endelevu ya dunia wakati wa Semina ya Wabunge kuhusu malengo hayo mjini Dodoma.
Pichani juu na chini ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki kwenye semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Mbunge wa viti maalum CCM Dodoma, Fatma Toufiq akichangia hoja wakati wa semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile akitoa maoni wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata akijengea hoja suala la usawa wa kijinsia wakati semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Segerea,Mhe: Bonnah Kaluwa (wa pili kushoto) wakati wa semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akifurahi jambo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Leonidas Gama ndani ya ukumbi wa bunge wa Msekwa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimchagulia Malengo ya Dunia ya Maendeleo Endelevu (SDGs) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwa ajili ya kumbukumbu za picha. Kushoto ni Afisa Habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Owen Mwandumbya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisapoti lengo namba 16 na 10 kati ya Malengo ya Dunia 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson katika picha ya pamoja na bango lenye rangi mbalimbali zinazowakilisha Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya dunia nje ya ukumbi mdogo wa Bunge mjini Dodoma.
Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) wakiwa na mabango yenye Malengo Mapya 2 kati ya 17 ya dunia wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo Bungeni Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mama Sophia Simba.
Afisa Habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Owen Mwandumbya akipozi na lengo la 9 la Maendeleo Endelevu.
Wabunge Mhe. Margaret Sitta (Kushoto) na Mhe. Najma Murtaza Giga, Mwenyekiti wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja mabango yenye rangi za Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo nchini iliyofanyika Bungeni, Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipozi na Malengo mbalimbali ya Maendeleo Endelevu baada semina.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na bango linalowakilisha Malengo ya Maendeleo ya Endelevu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kumalizika kwa semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura akisalimiana Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) wakati wa semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Owen Mwandumbya nje ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa.
No comments:
Post a Comment