Sunday, June 5, 2016

MUHAMMAD ALI ENZI ZA UHAI WAKE

Hapa ilikua mwaka 1980 Muhammad Ali akiongea na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa Dar alipokuja Tanzania kushininiza Tanzania isusie mashindano ya Olympic yaliyofanyika Urusi mjini Moscow. Pamoja na Tanzania kukataa shinikizo hilo, Muhammad Ali alipokelewa kwa heshima kubwa. Moja ya waandishi waliozungumuza na Muhammad Ali alikuwepo Dr. Hamza Mwamoyo ambaye kwa sasa ni mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya sauti ya America jijini Washington, DC.
Muhammad Ali akimpeba enzi hizo mtoto Iddi Alkhag akimtabiria kuwa atakua mpiganaji wa mchezo wa ngumi lakini katika kukua kwake Iddi Alkhag ni mchezaji wa mpira wa miguu anayechezea mpira wa kulipya Denmark wazazi wake mmoja akiwa Mtanzania ambaye ni Bahari Gangwe Khamisin Alkhag anayeishi Houston, Texas nchini Marekani na mama ni Mdenmark.
Iddi Alkhag akiwajibika katika mpira wa kulipwa nchini Denmark
[DSC04402.JPG]
Hapa Iddi Alkhag akikabidhi jozi 20 za viatu ma shini gadi za mpira wa miguu kwa aliyekua katibu wa TFF Bwn. Frederick Mwakalebela, siku mchezaji huyo alipokanyaga ardhi ya Tanzania kwa mara yakwanza baada ya miaka 30 alipozaliwa nchini Denmark, kulia ni baba yake Khamsini Alkhag akiwa na mkewe mama mitindo Asya Idarous Khamsini (kushoto) (picha na Michuzi)

No comments: