Sunday, June 12, 2016

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI MBALIMBALI WILAYA YA MBINGA VIJIJINI, RUVUMA

Mkurugenzi wa Halmashauriya ya mji wa Mbinga, Oscar Yapesa (kushoto) akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga vijijini, Venance Mwamenge mara baada ya kumaliza mbio zake katika mji wa Mbinga, jana.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, George Mbijima (kulia) akikabidhi Chandarua chenye dawa kwa mkazi wa kijiji cha Mbuji kata ya Mbuji wilayani Mbinga, Sailice Komba ikiwa ni mpango wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa wananchi wake. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbinga vijijini, Venance Mwamengo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, George Mbijima akiangalia ubora wa meza na madawati katika kijiji cha Mbuji wilayani Mbinga kabla ya kusambazwa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani humo.
Mratibu wa Elimu katika kata ya Litura Halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini mkoani Ruvuma, Nicodem Hyera akijaribu kuwasha moja kati ya pikipii zilizotolewa na Halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kuwawezesha waratibu elimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu ziweze kuwasaidia kufuatilia maendeleo ya elimu kwa shule za msingi na sekondari wilayani Mbinga. Picha zote na Muhidin Amri

No comments: