ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 29, 2016

NANI WA KUMGUSA LUGUMI?

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu
By Sharon Sauwa, Mwananchi ssauwa@mwananchi.co.tz

Dodoma. Ripoti ya sakata la mkataba wa Kampuni ya Lugumi Enteprises na Polisi, ambayo ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge, sasa itawasilishwa mkutano ujao.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Hilary Aeshi (picha juu) alisema ripoti hiyo itaunganishwa katika taarifa za kamati ambazo kwa utaratibu huwasilishwa kwenye mkutano huo.

Hadi wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akifanya ukaguzi wa mkataba huo wa Sh37 bilioni uliosainiwa mwaka 2013, ni vituo 14 tu vilivyokuwa vimefungwa mashine hizo, lakini mzabuni alishalipwa Sh36 bilioni.

No comments: