Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya Mahale,Mhifadhi Romanus Mkonda akizungumza juu ya ujenzi wa madaraja ulioanza katika barabara ya kuelekea katika hifadhi hiyo.
Wanahabari wakimsilikiliza Mhandisi kutoka kampuni ya ujenzi ya Lilangela inayojenga daraja la Lagosa katika barabara ya Buhingu wilayani Uvinza ,Marango Ngose alipokuwa akizungumzia juu ya ujenzi huo unaofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kibao kinachoonesha taarifa mbalimbali juu ya ujenzi wa daraja hilo.
Baadhi ya mafundi wakijaribu kuchimba udongo katika eneo la mto Lagosa ambako daraja hilo linajengwa.
Baadhi ya malighafi zinazotumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zikiwa eneo la ujenzi.
Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili kuta tatua changamoto ya wananchi katka vijiji hivyo kuvuka kwenda upande mwingine ambako kwa sasa wamekuwa wakilazimika kuvuka katikati ya mto huku wakiwa wamebeba vyombo vyao vya usafiri na hata mifugo imekua ikipita katika mto huo.
Ari kadharika kina mama na watoto kwa sasa wamekua wakilazimika kwenda kupata huduma ya maji upande wa pili wa mto huo na kwamba wanalazimika pia kupita ndani ya mto huo ili kuvuka kwenda katika makazi yao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwa ameongozana na wanahabari wakitoka katika eneo kunako jengwa daraja hilo.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog aliyeko Kigoma.
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetoa Sh.
Milioni 584 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ikiwa ni njia
moja ya kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Milima ya Mahale
vilivyopo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Baadhi ya wananchi wanaoishi katika vijiji vya
Lukoma na Igalula wanakabiliwa na
changamoto ya barabara jambo linalowafanya washindwe kufanya shughuli zao za
kimaendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea vijiji hivyo vilivyoko mwambao mwa zimwa Tanganyika ,Mkuu wa idara ya ujirani mwema ,Mhifadhi Romanus Mkonda aliyataja madaraja hayo kuwa Lagosa
na Lukoma.
“Daraja la Lagosa linatumia Sh. Milioni 296 wakati
lile la Lukoma litatumia Sh. Milioni 288,” alisema.
Alisema lengo
la TANAPA ni kusaidia
jitihada za serikali
za kuimarisha mawasiliano
ya barabara katika
ukanda huo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Iwapo barabara hiyo itapitika itarahisisha usafiri
na usafirishaji kwa
wananchi wa ukanda
huu na pia Hifadhi
yetu itaweza kupata watalii wengi kwa
sababu usafiri uliopo sasa hivi ni wa maji na Ndege pekee,” alisema.
Hata hivyo, alisema iwapo miundombinu hiyo ya
barabara itakamilika itaepusha gharama kubwa ambazo Hifadhi inaingia kwa ajili
ya kwenda mjini kununua vitu mbalimbali vya hifadhini.
Aliongeza kuwa barabara hiyo itawasaidia wananchi
hao kupata huduma mbalimbali zinazopatikana nje ya eneo lao ikiwa ni pamoja na
kusafirisha mazao na kuyapeleka masoko ya nje.
“Kwa mfano tunapotaka kwenda mjini tunatumia Boti
ambalo linatumia Lita 1000 za petroli kwenda na kurudi na oil lita 40...hivyo
iwapo barabara zitakamilika gharama hizi zitapungua,” alisema.
Pia, alisema barabara hizo zikikamilika utalii
utaongezeka na kuliongezea taifa pato.
Aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/17, TANAPA
imetenga Sh. Milioni 500 kwa ajili ya kujenga madaraja ya Nkonkwa na Igalula
yaliyopo vijijini hapo.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Igalula, Mussa
Matililo alisema iwapo madaraja hao yatakamilika itawarahisishia wananchi wa
maeneo hayo katika shughuli zao za kilimo.
“Pia, itarahisisha mawasiliano ya kijiji kimoja
kwenda kijiji kingine kwa sababu kwa sasa mawasiliano yamekuwa magumu kutokana
nah ii mito miwili,” alisema.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment