Sunday, June 5, 2016

RC AAGIZA MKURUGENZI HANANG AFIKISHWE KORTINI

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera ameagiza aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hanang’ Filex Mabula na Aliyekuwa mweka hazina wa Halmashauri hiyo Matonya Mizengo wafikishwe mahakamani kujibu mashitaka ya upotevu wa Sh932 milioni.
Akizungumza juzi wilayani Hanang Dk Bendera alisema taarifa ya uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zilizokuwa zinawakabili Mabula na Mizengo waliosimamishwa tangu Aprili 6 mwaka huu, zimewaingiza hatiani.
Dk Bendera alisema kamati hiyo ilibaini kuwa Mabula na Matonya wameisababishia halmashauri hiyo madeni ikiwamo hospitali ya wilaya (Tumaini) inayodaiwa na Bohari ya Dawa (MSD) Sh34.606 milioni hivyo wamepoteza sifa za utumishi na wafikishwe mahakamani.

No comments: