Thursday, June 2, 2016

Ripoti: Kifo cha Prince kilitokana na "ovadozi" ya madawa ya Fentanyl

Photo Credits: Hot102.9.com
Ripoti ya awali ya uchunguzi wa kitabibu kuhusu kifo cha mwanamuziki Prince Rogers Nelson maarufu kama Prince inaonyesha kwamba msanii huyo alikufa kutokana na "ajali" ya kujidunga madawa ya Fentanyl.
Prince alifariki Aprili 21 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 57.
Dawa za Fentanyl hutolewa na madaktari kwa wagonjwa wa saratani. Dawa hizo zinazidi kujitokeza kwenye vifo vingi vinavyotokana na kujidunga madawa nchini Marekani.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya udhibiti wa madawa nchini Marekani, Fentanyl inasemekana kuwa na nguvu / madhara mara 25 mpaka 50 kuliko dawa za Heroin, na ni zaidi ya mara 50 mpaka 100 ya madhara ya Morphine.
Prince alikutwa hajitambui katika "lift" iliyopo kwenye eneo lake linalojulikana kama Paisley Park, huko Chanhassen, Minnesota ambako pia ndipo yalipo makazi yake na studio ya kurekodia muziki.
Hii ni ripoti iliyotolewa hii leo. Ripoti kamili ya uchunguzi wake (Full Autopsy and toxicology report) havitowekwa wazi.

1 comment:

Anonymous said...

Muda wote huo mlikua wapi hamkutoa ripoti, I don't believe you kwendraaaaa