Iftar June, 18,2016 Mt.Vernon-NY yafana sana. Mwenyekiti wa New York Tanzania Community anapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wanajumuiya wote kwa kufanikisha shughuli hii.Tunashukuru wote waliofika kujumuika , shukrani sana . Shukran kwa mashekhe, waalim na wakinamama kutoka Springfield MA, toka Connecticut, toka Pennsylvania, toka New Jersey, toka New York pamoja na toka Houston TX .
Shukran kwa kamati ya maandalizi wamefanya kazi kubwa sana kufanikisha hili , Wajumbe wa kamati ya iftar ; Seif Akida, Fuad Khamis ,Amir Kius, Bahia Maundi, Mwanamkasi aksante kwa muda na sadaka zenu pia kuhakikisha utamaduni -desturi unafuatwa. Mwanamkasi nifikishie shukrani za dhati kwa akina mama walishiriki mapishi.Bila kuwatenga wakina baba waliopika Shukran sana waungwana.
Shukran kwa waliotoa eneo la shughuli .Mwezi wa toba, mwezi wa kutoa sadaka , mwezi wa kusamehana ....tufungue milango ya maelewano na swaumu zipate kuswiii! Wengi wamejitolea shughuli hii pokea shukrani zetu majina tukiweka mengi
Kwa ufupi shughuli ilifana chakula makini , na mawaidha dawaa makini toka kwa walimu Tuendelee na mshikamano wetu.
#The state of our community is Strong.
Sylvester Mwingira,
Mwenyekiti NYCT.
Sylvester Mwingira,
Mwenyekiti NYCT.
Akina baba wakipata ukodak
Mwenyekiti wa NYCT akipata ukodak na Mwenyekiti wa CCM Tawi la New York Bwana Seif Akida.
Bahia akipata ukodak na mke wa mkuu wa wilaya ya Springfield.
Maanjumanti yalikuwa ya kutosha sambamba na vinywaji.
Mwanamkasi kulia kiongozi wa mapishi akipata ukotak
1 comment:
masha Allah great pictures na mmependeza nyote masha Allah
Post a Comment