Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu. Ikiwa jana Mbunge huyo alihojiwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi cha Kanda maalumu ya Dar es Salaam na kutupwa Rumande mara baada ya kukosa dhamana.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwasiri mahakamani leo.
Kwa habari zilizotufikia hivi punde kutoka mahakamani inasema kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana na ameamuriwa kutosafiri nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment