Friday, June 3, 2016

UFAFANUZI JUU TIMUA TIMUA YA WANAFUNZI

By Malisa GJ

Baada ya timua timua ya wanafunzi walioko vyuoni imeonekana kuna watu wanajadili vitu wasivyovijua vizuri. Watu wengi wanaonekana kuchanganya kati ya wanafunzi waliotimuliwa UDOM na wale waliotimuliwa vyuo vingine kwa kukosa sifa. Ni vizuri wakati wa kujadili tukaelewa tunajadili kundi gani kati ya haya mawili.

#KUNDI_LA_KWANZA ni wale waliopata division one hadi three na wakapata alama "A" au "B" kwenye masomo ya Sayansi (Physics, Maths, Chemistry, Biology). Hawa walidahiliwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa program maalumu ya miaka mitatu ya kupata diploma ya ualimu wa sekondari.

Utaratibu huu haukuanzishwa na wanafunzi hawa. Ulianzishwa na Rais JK na kupigiwa vigelegele na wafuasi wote wa CCM. Leo JPM anaona ni utaratibu wa hovyo na anawaadhibu wanafunzi kwa kuwafukuza. Cha ajabu wafuasi walewale waliomshangilia JK akianzisha mfumo huu ndio haohao wanaomshangilia JPM akiufuta. Huu ni uzwazwa wa shahaha ya juu kabisa ya uzamivu uliobobea (PhD with gigantic Experiece).

Kwanini tunawahukumu watoto wasio na hatia? Yawezekana tunahitaji marekebisho ktk mfumo wa elimu lakini si kwa style hii. Nadhani kama JPM angekua na busara angesubiri watoto hawa wamalize kisha ndo aufute huu mfumo. Lakini kuufuta sasa hivi wakati ameshawapotezea miaka mitatu ni ukatili. Wanafunzi hawa wangeendelea form five (sifa wanazo) kwa sasa wangekua first year chuo kikuu. Kwahiyo wanafunzi waliotimuliwa UDOM hawajafeli kama inavyoenezwa.

Na kama mfumo huu ulikua haufai kwanini vijana wa CCM mlimshangilia JK alipokua anauanzisha? Si mngemwambia tu wazi kuwa Mzee hii si sawa. But mlipiga makofi kumshangilia halafu leo amekuja mtu mwingine ameufuta mnamshangilia tena?

Hivi vijana wa CCM hamnaga "ujasiri" wa kumkosoa kiongozi awapo madarakani hadi msubiri atoke? Kwa hali hii nina wasiwasi hata JPM akiondoka akija mwingine akarudisha mfumo huu mtamshangilia tena na kuona JPM alifanya ugoro. Kwanini hamna national interest, badala yake mmekuwa wapiga zumari wa Rais aliyeko madarakani hata kama amekosea mnamshangilia tu?

Anyway. Lakini je ni dhambi mtu wa kidato cha nne kwenda chuo kikuu? Je Utaratibu huu ni mpya nchini? Jibu si dhambi. Na utaratibu huu si mpya. Issue sio mtu kuwa chuo kikuu, issue ni anasoma nini huko chuo kikuu. Hivi mhitimu wa kidato cha 4 akienda chuo kikuu akasomea "certificate" tutashangaa? Mbona wapo wengi tu wamejaa huko UDSM, UDOM, SAUT, IFM, CBE, Mzumbe wamesoma "certificate" mwaka mmoja na baadae Diploma na hata "degree" lakini hatuwashangai?

The same applies kwa hawa vijana wa UDOM. Wamemaliza form four wamefaulu vzr wakaenda kusomea Diploma ya ualimu miaka mitatu. Ni sawa na kusema mwaka mmoja wamesoma certificate (foundation course), miaka miwili "diploma". Je hapo kuna ubaya gani?

Eti tunawashangaa na kuwaona wa ajabu. Kabla hatujawashangaa vijana hawa wameendaje chuo kikuu bila kufika form six, tumshangae kwanza Prof.Mark Mwandosya amekuaje Profesa wakati HAIJUI form five wala six.

Mwandosya alipomaliza form four pale Malangali sekondari mwaka 1968, alienda DIT kusoma certificate ya Engineering (FTC) kisha akajiunga na Aston University huko Uingereza kwa BSc. (Engineering). Mbona huyu hatumshangai tunashangaa hawa watoto wa UDOM? Kutokwenda form five sio kitu cha ajabu. Na tuna wataalamu wengi tu hawajapita form five lakini wanafanya vzr sn.

#KUNDI_LA_PILI
Hiki ni kundi la vijana wapatao kama 400+ waliokua wamedahiliwa vyuo vikuu mbalimbali nchini wakitokea form four na wamefeli halafu wanasoma degree wakati hawana "foundation course" yoyote ya certificate wala diploma. Hawa wametimuliwa na mama Ndalichako. Nimeona orodha yao wengi ni watoto wa vigogo. Ajabu walikua wakipewa mikopo 100%. Mmoja wao ni Scholastica Nchimbi aliyekua chuo Kikuu cha St.Joseph akisomea Civil Engineering. Anadaiwa kuwa na division four ya point 29 na hajasoma foundation course popote, lakini alikua chuo kikuu na ana mkopo 100%.

Hawa wa kundi la pili naunga mkono watimuliwe au wahamishiwe level za chini wanazozimudu. Kama wanasoma degree wahamishiwe certificate. Lakini lazima tujiulize waliingiaje? Kama ni watoto wa vigogo it means kuna matumizi mabaya ya madaraka hapa, hivyo viongozi waliohusika ni muhimu wawajibishwe. Pia waliowadahili nao wachukuliwe hatua. Vyuo vilivyowapokea navyo viwajibishwe.

Lakini cha ajabu ni kuwa viongozi wenye tuhuma hizi "hawagusiki". Mmoja wa viongozi ambaye inadaiwa mwanae yupo kundi hili ni RC mmoja ambaye amepewa ubunge juzijuzi. Hivi kiongozi kama huyu aliyeshawishi mwanae ajiunge chuo kikuu wakati ana division four ya 29 anapewaje zawadi ya ubunge kama nyongeza?

Kwa hiyo tunapojenga hoja tujue kuna makundi mawili yanaguswa. Usije kuchanganya vijana wa UDOM (Magenius) na watoto wa kina Mu-longolongo (vilaza) kwa kuwa wote wametimuliwa. Usiwavictimize vijana wa UDOM kwa kuwafananisha na watoto wa mawaziri waliotimuliwa huko St.Joseph na kwingineko. Ni dhambi.!

Malisa G.J

3 comments:

Anonymous said...

Wewe ndiyo hukuelewa, ni kwamba kina wanafunziwasio na sifa wengi kwahiyo wanachujwa ili walio na sifa waendelee na masomo na wale wengine wstafute vyuo kulingana na ufaulu wao. Unetumia muda mrefu kuelezea jambo ambalo mwenyewe hukulielewa. Acha uchocgexi.

Anonymous said...

najuta kupoteza muda wangu kusoma,mimi nilivyosoma kichwa cha habari nilifikirimwandishi ni mtu mwnye uelewa kumbe naye ni shabiki,jamani jpm sio kwamba kawafukuza au kafuta hiyo programu.ila program imeharibiwa na watu wenye uchu walee waliokuwa wakiongozwa na kikwete.yaani profesor kutoka chama cha ACT wazalendo alifanya uchambuzi na akawapa taarifa kuwa wanafunzi wanaotakiwa kudairiwa ni 1800 tu wenye uchu wakadairi 7700 just check the differenceukiacha hiyo wengi hawana sifa wamepelekwa pale ni vilaza tu na waliyofauru wameachwa nyumbani watoto wa mkulima JPM sio fara kama wewe mwandishi usiyekuwa na taaluma ya kupata habari kutoka kwenye source mwenzio kafanya utafiti hajakurupuka.na akasema wanafanya uchunguzi wenye sifa watarudi wasio nazo waendee kleruu huko.sasa majibu yakitoka ndo utahakikisha ni jinsi gani wasionasifa walivyowengi.sijajua utakuja kuandika tena,yaani waandishi wa Tanzani hewa acha mimi nafikiri magufuri awageukie na waandishi hewa maana tumechokaaaa

Anonymous said...

yaani hii blog ya vijimambo nimeanza kuichukia,hivi huyu mwandishi wa wapi jamani haelewi hivi unasikilizaga taarifa au unakurupuka?umejuaje wanafunzi 7700 wengine sio hewa je umefanya uchunguzi?pia habari za kufutwa program umeipata wapi?vijimambo why mnaruhusu upotoshwaji wa namna hii?hii program haijafutwa,watoto wataendeleaje kukaa chuo na wakati hawafundishwi walimu wamegoma miezi miwili.mimi nachoona selikali ya jpm imekosea ni ile kutoa masaa 24 kama kweli ilifanya hivyo si vzr ila twende na fact hapa chuo wengi wana 4 ila watoto wawakubwa