ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 20, 2016

YANGA IMEPOTEZA MECHI YAKE YA KWANZA KATIKA HATUA YA MAKUNDI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

Klabu ya Yanga usiku wa kuamkia leo imecheza pambano lake la kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya MO Bejaia ya Algeria. Katika mchezo huo Yanga walifungwa goli moja dakika ya 20 na likadumu hadi mwisho wa mchezo.
Matokeo hayo yanaifanya MO Bejaia ishike nafasi ya pili katika kundi hilo, nyuma ya TP Mazembe ambayo iliifunga Medeama ya Ghana 3-1 katika mchezo wa kwanza mjini Lubumbashi Jumapili, wakati Yanga inashika nafasi ya tatu.
Mechi zijazo za kundi hilo, Yanga watakuwa wenyeji wa Mazembe Dar es Salaam na Medeama wataikaribisha Mo Bejaia.

No comments: