Advertisements

Wednesday, July 20, 2016

AMUUA DADA AKIDAI ANAPENDELEWA

By Gasper Andrew, Mwananchi gandrew@mwananchi.co.tz

Singida. Mkazi wa Kijiji cha Misuna Wilaya ya Mkalama, anadaiwa kumuua mwanafunzi wa darasa la nne wa Shule ya Msingi Mgungira, Wilaya ya Iramba, Sharifa Juma (12) kwa kumkata kwa panga shingoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka amesema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro kati ya mwanafunzi huyo na mtuhumiwa kwa madai kuwa baba yao alikuwa akimpendelea Sharifa wakati ni mtoto wa kambo.

“Tunamshikilia kwa mahojiano baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani,” amesema.

Wakati huo huo; Sedoyeka amesema mkazi wa Karakana, Patrick John (34) amekutwa amekufa barabarani Jumamosi iliyopita saa 12 jioni.

Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitiawww.epaper.mcl.co.tz

No comments: