Advertisements

Wednesday, July 20, 2016

DC KAKONKO AONYA WANUNUZI WA PAMBA KUCHEZEA MIZANI

 
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala ( watatu kushoto) akimsikiliza Wakaa wa Vipimo Wilayani humo, Laurent Kabikiye (aliyeshikilia mzani) wakati wa uhakiki wa mizani hiyo.
 
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (mwenye koti kushoto) amewaonya wanunuzi wa Pamba Wiayani humo kuchezea mizani wanazopia zao hilo wakati wa ununuzi kwa wakulima kwa lengo a kuwapunja wakulima na kujinufaisha zaidi. Source:Father Kidevu Blog

Kanali Ndagala aliyasema hayo leo wakati akizindua msimu mpya wa ununuzi wa Pamba aioufanya katika Kijiji cha Kanyonza na kusema kuwa wafanya biashara wahakikishe kuwa mizani wanayotumia haijachezewa kwa namna yeyote na iwe imefanyiwa ukaguzi na wakala wa vipimo.

“Leo tunazindua ununuzi wa wa zao la Pamba katika maeneo yetu, lakini nitoe angalizo kwa wanunuzi kuhusiana na mizani mtakayoitumia kununulia Pamba isiwe imechezewa na kuwapunja wakulima,”alisema Kanali Ndagala.

Aidha Kanali Ndagala aliwatahadharisha wakulima kuhakikisha pamba wanayoileta sokoni ni Pamba safi na siyo iliyo wekwa maji au vitu vingine vyotote kama mchanga kwa lengo la kuongeza uzito na kujipatia manufaa.

Kanali Ndagala alisema kitendo cha kuweka maji au vitu vingine katika Pamba ni kuharibu bidhaa hiyo na kuharibu soko kwa ujumla la zao a pambamba na kutawafanya wanunuzi kusitisha ununuzi huo katika maeneo yao.

No comments: