Advertisements

Monday, July 11, 2016

Katavi kinara wa mimba za utotoni

By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mkoa wa Katavi ndio unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimba wakiwa na umri mdogo.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, Mkurugenzi wa NBS Albina Chuwa alisema takwimu zinaonyesha mkoa huo unaongoza kwa asilimia 36.8, Tabora 36.5 na Simiyu 32.1 huku Dar es Salaam ukiwa mwishoni kwa asilimia 12.

kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la watu duniani (UNFPA), Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu zinazoongoza kwa tatizo hilo barani Afrika.

Kutokana na hali hiyo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu aliitaja jamii kutoendeleza vitendo vya udhalilishaji kwa watoto wa kike, huku akidai kuwa lazima hatua za haraka za kukabiliana na tatizo hilo zifanywe.

Awali Mkurugenzi wa huduma za afya wa Shirika la Maria Stopes, Dk Joseph Komwihangiro alisema ili kupambana na hali hiyo lazima wasichana wapewe elimu kuhusu masuala ya uzazi ili waweze kujilinda na ndoa za utotoni.

Takwimu zinaonyesha zaidi ya asilimia 10 ya wasichana walio na umri mdogo wameanza kutumia njia za uzazi wa mpango.

Mwisho.

No comments: