Advertisements

Saturday, July 9, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AWASILI JIJINI MBEYA TAYARI KWA KUFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA UASKARI MAGEREZA, CHUO CHA MAGEREZA, KIWIRA


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akipokea Salaam ya Kijeshi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP. Dhahiri Kidavashari alipowasili Julai 8, 2016 katika Uwanja wa Ndege wa Songwe tayari kwa kufunga Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza leo Julai 9, 2016 katika Chuo cha Magereza, Kiwira Mkoani Mbeya (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja (kulia) akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, Jijini Mbeya jana jioni Julai 8, 2016 (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: