Advertisements

Sunday, July 31, 2016

MBOWE AWASILI POLISI KUHOJIWA, LOWASSA AZUIWA KUINGIA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema), Freeman Mbowe leo july 31 amewasili makao makuu ya jeshi la polisi kuitikia wito wa kuhojiwa na jeshi hilo huku hali ya usalama ukiwa imeimarishwa kabla na baada ya Mbowe kuwasili .
 
Mbowe akiwa na msafara wa magari nane walikutana na ulinzi huo makali ambapo magari ya Mbowe na Wakili Peter Kibatala ambaye alikuwa na Tundu Lissu ndio yaliruhusiwa kuingia.

Gari la Edward Lowassa na viongozi wengine wamezuiwa kwenye geti la kuingia kituoni hapo ambapo geti hilo limezibwa na gari la maji ya kuwasha ili kutoruhusu gari yoyote kutoka au kuingia.

No comments: