Advertisements

Saturday, July 30, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA MKOANI MWANZA AANZA ZIARA ZA KUKAGUA MIUNDOMBINU JIMBONI HUMO

Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula (katikati), jana amefanya ziara ya kukagua Ukarabati wa Miundombinu ya barabara, mitaro na madaraja katika Kata ya Kirumba Jimboni humo ikiwa ni mwanzo wa ziara zake katika Kata zote za Manispaa ya Ilemela ili kujionea namna ukarabati wa mbiundombinu ya barabara unavyoendelea.

Kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika kutokana na mvua ambapo miongoni mwa barabara zinazokarabatiwa katika Kata ya Kirumba ni barabara ya Villa, Kabuhoro, CWT-Sabatho.
Na BMG
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (wa nne kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.
Mitaro katika barabara ya Villa inaendelea kukarabatiwa ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua na kusababisha adha kubwa kwa wananchi.

Hii ni barabara ya CWT-Sabatho, awali ilikuwa haitamaniki kwani ilikuwa ni mashimo tupu. Lakini sasa inapitika vyema na kilichosalia ni ukarabati wa mitaro ili mvua ikinyesha isiweze kusababisha uharibifu wa ukarabati huu.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (wa tatu kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.
Namna miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Ukaguzi wa miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Pia kuna ujenzi wa daraja katika barabara ya Kabuhoro Ziwani ambapo kulikuwa na adha kubwa kwa wananchi ambapo ukarabati huu unaleta ahueni kwa wakazi wa eneo hio pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

Aliagiza ukarabati wa mbiundombinu ya barabara kukamilika haraka kabla msimu wa mvua haujaanza na kwamba Manispaa ya Ilemela imetenga Shilingi Milioni 625 ikiwa ni fedha za mfuko wa dharura na shilingi Milioni 146 ambazo ni fedha za mfuko wa barabara, fedha zote ikiwa ni kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (mwenye miwani) akiteta kidogo na wakazi wa Kata ya Kirumba alipotembelea Kata hiyo ili kujionea ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata hiyo.
Katibu wa Mbunge, Heri James (mwenye kofia) ambapo alisema ofisi ya mbunge itahakikisha ahadi zilizotolewa na mbunge wakati wa kampeni zinatekelezwa ikiwemo suala la upatikanaji wa maji na ukarabati wa miundombinu.
Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika kutokana na mvua.
Diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, ambapo alibainisha kwamba barabara za Kata hiyo zilikuwa zimeharibika sana kutokana na mvua zilizonyesha mwishoni mwanza mwaka jana. 

Alishukuru ushirikiano baina yake na wananchi wa Kata yake, ofisi ya mbunge pamoja na halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kwamba juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuwafikishia wananchi maendeleo zimepokelewa vyema na wananchi huku akiwasihi kuitunza vyema miundombinu hiyo.
Mmoja wa wakazi wa Kirumba akieleza adha waliyokuwa wakiipata wakazi wa Kata hiyo kabla ukarabati haujafanyika ambapo aliongeza kwamba ni vyema ukarabati huo ukaendelea kufanyika hususani katika ujenzi wa mitaro ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua ikwemo kuharibu miundombinu ya barabara kutokana na kukosekana kwa mitaro.
Mkazi wa Kirumba akitoa shukurani zake kwa ukarabati unaofanyika katika barabara za Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Tazama Hapa Miundombinu Ilivyokuwa Awali

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imeanza ukarabati wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha changarawe pamoja na mikakati ya ujenzi wa baadhi ya barabara kwa kiwango cha lami.

Akikagua zoezi la ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata ya kirumba, Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula, ametaka ukarabati wa miundombinu hiyo ikiwemo mitaro, kukamilika mapema kabla msimu wa mvua haujaanza ili kuepukana na athari za mvua.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano, hali ya miundo mbinu ya barabara katika jimbo hilo itakuwa katika hali nzuri na hivyo kupunguza kero ya ubovu wa miundombinu ambayo imekuwepo kwa muda mrefu katika Manispaa ya Ilemela.

Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, amesema Manispaa hiyo imetenga shilingi Milioni 625 zilizotokana na fedha za mfuko wa dharura na barabara kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo japo amebainisha kwamba bado fedha hizo hazitoshi hivyo ni vyema serikali ikaendelea kutenga fedha zaidi kwa ajili ya kutekeleza ukarabari huo.

Wakati ukarabati huo ukiendelea, diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, amewataka wananchi kutunza vyema mbiundombinu ya barabara inayoendelea kukarabatiwa ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mitaro.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kirumba, wamepongeza juhudi za ukarabati wa miundombinu ya barabara zinazofanyika katika Manispaa ya Ilemela na kuongeza kwamba ni vyema juhudi hizo zikandelea ili kumaliza kero zilizokuwepo awali.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela, yuko katika mwendelezo wa ziara katika Kata zote 19 za Manispaa ya Ilemela ili kujionea ukarabati wa Miundombinu ya barabara ambayo ni pamoja na ujenzi wa mitaro na madaraja ambao unaelezwa kuleta ahueni kwa wananchi wa Manispaa hiy ikizingatiwa kwamba awali hali ya miundombinu ya barabara awali haikuwa ya kuridhisha.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play Hapo Chini.

No comments: