Advertisements

Friday, July 29, 2016

MISS TANGA KUFANYIKA LEO IJUMAA KWENYE UKUMBI WA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT

Warembo wanaowania Taji la Mrembo wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016) wakiwa kwenye pozi katika hotel ya Tanga Beach Resort kutakapofanyika shindano hilo Ijumaa leo.
Warembo hao wakiwa kwenye picha ya pozi 
Warembo wanaowania Taji la Urembo Mkoa wa Tanga(Miss Tanga 2016) ambalo linaandaliwa na Kituo cha Radio cha TK FM cha Mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wakiwa kwenye picha ya mapozi 
Mratibu wa Shindano ya Miss Tanga 2016,Mboni Muya akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusiana na maandalizi ya kuelekea shindano hilo 
Baadhi ya Warembo wakimsikiliza Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini Sinza,Beny Kisaka alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuitembelea kambi ya warembo hao wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Nassoro Makau 
Warembo hao wakimsikiliza Mratibu wa Shindano ya Miss Sinza 2016 ambaye aliitembelea kambi hiyo jana
Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini,Benny Kisaka akitoa nasaha kwa warembo wanaotarajiwa kushiriki kinyang'anyiro cha kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016 )itakayofanyika Ijumaa leo kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.
Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini,Benny Kisaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga Ijumaa
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments: