Advertisements

Friday, July 22, 2016

MUGABE APATA MPINZANI

Rais Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe, wakifurahia jambo

Chama cha askari wa zamani waliopigana vita nchini Zimbabwe, ambao wamekuwa kiungo muhimu katika uongozi wa rais Robert Mugabe na wakati mwingine wamekuwa chanzo cha vurugu kutokana na wanavyomuunga mkono rais huyo.

Ingawa kuna taarifa kutoka nchini Zimbabwe zikiarifu kwamba maveterani hao wameamua kutoa waraka wenye kuonesha msimamo wao kwamba kuanzia sasa hawatamuunga mkono tena rais huyo.

Chama hicho kinamshutumu rais Mugabe kwa tabia zake za kidikteta ,kuongoza kwa matakwa yake, na utawala mbovu ,ingawa haijafahamika wazi mpaka sasa ikiwa askari wote wa zamani wamekubaliana juu ya tamko hilo lililotolewa chini ya mwavuli wa chama.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na mkanyiko wa mawazo miongoni mwa wa Zimbabwe kila uchao kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili nchi hiyo kwa sasa.

Kwa sasa rais Robert Mugabe ana mika tisini na miwili,na kwa baadhi ya vikundi wakati fulani ndani ya uongozi wa chama cha Zanu-PF chama wamehusika katika mfululizo wa mapambano kama hayo ili kuinusuru Zimbabwe.

BBC

No comments: