Advertisements

Friday, July 22, 2016

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI ATEMBELEA CHUO CHA USAFIRISHAJI

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho kukagua miundombinu yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege na urubani alipotembelea Chuo cha Usafirishaji NIT.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani moja ya kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi wa ndege alipotembelea maktaba ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mtambo unaopima magari ili kujua ubora wake kabla ya kuanza kutumika hapa nchini alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT.

(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo)

No comments: