ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 27, 2016

PICHA: ZITTO NA MAALIM SEIF WALIVYOKUTANA KWENYE MKUTANO MAREKANI

Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wamekutana Katika Mkutano Maalum wa Viongozi wa Kisiasa Ulimwenguni (International Leaders Forum) ambao umefanyika jana  ‘Kwa Saa za Marekani’ Jijini Philadelphia.

Mkutano huo ulioandaliwa na asasi ya NDI ‘National Democratic Institute’, ni Sehemu ya matukio maalum kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention), Mkutano ambao utamthibitisha Bibi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais Kupitia Chama Hicho.


Zitto Kabwe Pamoja Na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim watakuwa Philadelphia mpaka Siku ya alhamis ambapo  mkutano huo unategemewa kumuidhinisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais wa Marekani kupitia Chama Hicho.

1 comment:

Anonymous said...

Watalii,tafadhali siasa za Hilary Clinton zilizopelekea kueneza maafa mashariki ya kati na hata pale Libya mkiondoka kurudi nyumbani mziache huko huko Philly. Kwanza huyo Hilary mwenyewe hakubaliki hata hapa Marekani na wamarekani waliowengi ana mazaga zaga tele bora hata Lowasa lol.