Mkurugenzi wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya Wachezaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein 'Machinga', wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa Tamasha hilo, Bahari Camari.
Mkurugenzi wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya Wachezaji wa zamani wa Simba, Moses Mkandawile, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa Tamasha hilo, Bahari Camari.
Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kulia) amkimkabidhi Tisheti Kipa wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, zitakazotumika kufanyia mazoezi siku ya Tamasha. (wa pili kushoto) Katikati ni Afisa Habari wa Property, Saleh na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada.
Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed, akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wachezaji wa zamani wa Vilabu vya Yanga na Simba, kuhusu Tamasha la jumamosi katika Uwanja wa Uhuru.
Na Ripota wa Sufianimafoto Blog,Dar
KAMPUNI ya Property International Ltd imedhamini bonanza la uzinduzi wa kitabu cha soka cha Safari ya Soka la Tanzania litakalofanyika Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika bonanza hilo la uzinduzi wa kitabu hicho litaambatana na maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya uhuru wa Algeria, ambalo litahudhuriwa na Waziri wa Habari Michezo na Utamaduni, Nape Nauye ambaye ataongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba.
Katika Bonanza hilo pia kutakuwa na mechi kadhaa ikiwemo maveterani wa timu za Simba na Yanga, mechi za vyombo vya habari pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali nchini Tanzania wataungana na kucheza na maveterani wa Simba na Yanga.
Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi za Property zilizopo mtaa wa Shauri Moyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo ya mipango miji Masoud Khalfan, alisema wamefurahishwa kushirikishwa katika mambo ya michezo na wako tayari kushiriki zaidi kwenye michezo.
“Kama tungepata mapema taarifa hizi za kudhamini, tungeweza kufanya makubwa zaidi katika bonanza hili, ila tumeamua kufanya tukio hilo kwa kiasi kidogo ili kutoa mchango wetu kwenye tukio hili kubwa na la kipekee kwenye historia ya soka la Tanzania la kuwaenzi wachezaji wa zamani, iwapo tutashirikishwa mapema katika mengine yajayo basi tunaamini tutweza kufanya zaidi ya haya” alisema Khalifan.
Naye balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed alizungumza katika mkutano huo, akisema wamefurahi kusherehekea miaka 54 ya uhuru wa nchi yao katika tukio hilo kubwa la kimichezo nchini.
“Ilkuwa tusherehekee miaka ya uhuru wa nchi tangu Julai 15, lakini tulipopta taarifa ya tukio la uzinduzi wa kitabu hicho na bonanza tuliamua kusogeza mbele hadi Jumamosi hii,” alisema Balabed.
Baadhi ya wachezaji mbalimbali wa zamani wa klabu za Simba na Yanga kama Kenneth Mkapa (Yanga), Mohamed Mwameja (Simba), Iddi Sulemani (Simba), Mohamed Hussein ‘Mmachiga’ (Yana na Simba) Tomas Kipese (Simba), Moses Mkandawile (Simba) walikuwemo kwenye mkutano na kila mmoja kutamba kumfunga mwenzake.
Katika bonanza hilo maveterani wa Simba watachezana na wale wa Yanga, kisha kutakuwa na mechi zingine kama E FM vs Bakheresa, Chanel Ten na Wasanii wa vichekesho, Orex na Umoja wa watuma salamu, kisha mechi ya mwisho ni maveterani hao wa Simba na Yanga kucheza na mabalozi hao.
Kitabu hicho cha Safari ya Soka la Tanzania kitakachozinduliwa kwenye bonanza hilo, kinahusu maisha na historia ya soka la Tanzania kuanzia mwaka 19926 hadi mwaka huu.
Mratibu Bahari Camari akizungumza.
Mchezaji wa zamani wa Simba Moses Mkandawile, akizunguma.
Beki wa zamani wa Yanga, Keneth Mkapa, akizungumza.
Kipa wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, akizungumza.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada (kulia) akizungumza na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed, kumfahamisha shughuli za kampuni hiyo, wakati alipofika Ofisini kwake leo mchana.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada akimuonesha Balozi huyo, baadhi ya Tuzo walizopata katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya mwaka huu, Sabasaba.
Mazungumzo.
Picha ya pamoja.
Balozi wa Algeria nchini Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa Vilabu vya Yanga na Simba,mara baada ya mkutano huo.
No comments:
Post a Comment