Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbalawa akizungumza kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28) unaoendelea jijini Dar es Salaam ukifahamika kama 2016 Mobile 360 Series – Africa ukihusisha wadau mbalimbali wa mawasiliano ya simu za mikononi.
Mkurugenzi Mkuu wa GSMA Bw Mats Granryad, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa GSMA Afrika Bw Mortimer Hope akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo. Tanzania ni miongoni mwa mataifa manane barani Afrika ambayo yana soko kubwa la simu za mikononi, ripoti mpya ya utafiti iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam imebainisha.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ijulikanayo;
‘Uchumi wa simu za mikononi: Afrika 2016’ iliyozinduliwa kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai
26-28) unahofahamika kama 2016 Mobile 360 Series – Africa ukihusisha wadau mbalimbali wa aina hiyo ya
mawasiliano, Tanzania imeungana na mataifa
ya Nigeria na Ethiopia ambayo kwa utatu
wao yanachukua zaidi ya theluthi moja ya soko la
aina hiyo ya mawasiliano barani Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi
ya watu nusu bilioni barani Afrika kwa
sasa wamejiunga na huduma ya simu za
mikononi huku kukiwa na idadi kubwa ya
watumiaji wa aina hiyo ya mawasiliano wanaohamia kwenye huduma ya internet
inayopatikana kwenye simu zao, utafiti mpya uliofanywa na na Umoja wa wadau wa
Mawasiliano ya simu za mikononi
Duniani ujulikanao kama GSMA
umebaini.
Ripoti hiyo pia iliangazia
mchango wa sekta ya mawasiliano ya simu hizo kiuchumi, ikiwemo ajira, ufadhiri
kwa umma (Public Funding) pamoja na mchango wa mawasilian hayo katika ukuaji wa
digitali na ushirikishwaji wa kifedha.
“Zaidi ya watu nusu bilioni
barani Afrika kwa sasa wamejiunga na huduma ya simu za mikononi, hatua ambayo
si tu inawaunganisha bali pia inatoa fursa kwao kuweza kupata huduma nyingine
kama vile huduma za afya, utambuzi wa kidigitali na huduma za kifedha,’’
alibainisha Mats Granryad, Mkurugenzi Mkuu wa GSMA. “Uhamiaji wa ghafla kwenda
kwenye matumizi ya internet ya simu miongoni mwa watumiaji inatoa fursa mpya kwa watumiaji, biashara,
serikali na kukuza mzunguko ambao mwaka jana uliongeza zaidi ya dola bilioni
150 kwenye uchumi wa bara la Afrika,’’
Uwekezaji kwenye mtandao (Network) na simu za kisasa (Smartphones)
kunachochea uhamiaji zaidi kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu.
No comments:
Post a Comment