Advertisements

Wednesday, July 13, 2016

UJIO WA BALOZI MASILINGI JIMBO LA MINNESOTA

Ndugu Watanzania wote mnaoishi jimboni Minnesota na miji ya jirani. Tunapenda kuwataarifu kuwa Balozi Wilson Masilingi ambaye ni Balozi wetu kutoka Washington DC atakutana na watanzania kwenye ukumbi wa African Development Center (ADC) siku ya Ijumaa, tarehe 07/22/2016 saa 11:30 jioni.
 
Anuani ya ADC ni:
 
1931 S 5th St, 
Minneapolis, MN 55454
 
Wote mnakaribishwa!
 
Ujio wa Balozi unaratibiwa na Uongozi wa DICOTA, Minnesota.

No comments: