Maduka mengi yanayouza filamu katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, yamefungwa baada ya mamlaka ya mapato Tanzania, TRA kuwataka wamiliki waoneshe mikataba ya usambazaji wa filamu hizo za nje.
Filamu hizo zinadaiwa kutolipiwa ushuru. Kwa mujibu taarifa ya Channel 10, baadhi ya maduka yamefunguliwa nusu huku wamiliki wakifanya biashara kwa kuibia.
Wafanyabiashara hao wamejitetea kuwa hawana mikataba ya usambazaji na kwamba filamu hizo zinapoingia nchini zinakuwa zimeshalipiwa ushuru.
Wakiongea kwenye mkutano na maafisa wa serikali, wafanyabiashara hao wamedai kuwa takriban maduka 40 yamefungwa. Wamesema kuwa suala la kuwa na mikataba na wamiliki wa filamu hizo ni kitu kisichotekelezeka.
No comments:
Post a Comment