Advertisements

Thursday, July 21, 2016

WANACHAMA WA REPUBLICAN WAMZOMEA SENETA TED CRUZ

Seneta wa Texas Ted Cruz amezomewa baada ya kushindwa kumuunga mkono Donald Trump kama mgombea urais kwa chama cha Republican, wakati akitoa hotuba yake kwenye mkutano mkuu wa kitaifa wa chama hicho huko Cleveland.

Katika hotuba yake hiyo Cruz aliishia kumpongeza Trump ambaye alikuwa ni mshindani wake mkuu katika kinyang'anyiro cha kupata kura za awali za wanachama wa chama hicho cha Republican.

Kundi la wanachama wenye hasiri walisikika wakisema “Tunamtaka Trump”, na kuongeza “Muidhinishe”, wakati Cruz alipokuwa akikaribia kumalizia hotuba yake hiyo katika mkutano huo.
Seneta Ted Cruz akiwapungia mkono wanachama wa Republican baada ya kukamilisha hotuba yake

No comments: