Advertisements

Monday, August 29, 2016

CHADEMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA KUAHIRISHWA OPERESHENI UKUTA.

CHADEMA inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu andiko linalosambazwa mitandaoni likimnukuu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa ameahirisha Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1.

Tunaomba umma upate taarifa sahihi kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya mkutano na waandishi wa habari mahali popote pale kuzungumzia kuahirisha Operesheni UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia maandalizi ya Septemba 1.

Kupitia taarifa hii, chama kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na Watanzania wote wazalendo na wapenda haki, kupuuza andiko linalosambazwa mitandaoni .


Msisitizo unaendelea kutolewa kuwa Operesheni UKUTA ambayo imelenga kusimamia utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi na kulinda sheria na maandalizi yanaendelea nchi nzima.

Imetolewa na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

2 comments:

Anonymous said...

Naona Mbowe anajaribu kupiga mateke upepo. Anajitahidi kujitutumua kwa jambo ambalo hata yeye mwenyewe anajua kuwa impact yake itakuwa very minimal.

Anonymous said...

hatuendi, nani akaumizwe wakti nyie mnakula viyoyozi.