ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 25, 2016

CHAMA CHA WALIMU TABORA CHAIDAI SERIKALI SHILINGI BILIONI 2.

Image result for walimu
Na Mussa Mbeho,Tabora.

Chama cha walimu mkoani Tabora kimeioba serikali kuwalipa walimu madai yao yote ambayo imekuwa akiahidi kuwapatia tangu mwezi wa kwanza ili waweze kujikimu kimaisha na kuwa na molali ya kuendelea kufundisha katika shule zao.

Akizungumza kwenye baraza la walimu lililofanyika katika ukumbi wa chama hicho mkoani hapa katibu wa chama cha walimu ARONE MASALU amesema kuwa walimu wanaidai serikali jumla ya shilingi bilioni 2.3 ambazo wamekuwa wakiahidiwa bila kulipwa kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

MASALU amesema kuwa fedha hizo wanazoidai serikali ni pamoja na mishahara,fedha za likizo,uhamisho na zile za kujikimu ambazo serikali imekuwa ikizitoa kwa ajiri ya walimu wapya wanaoajiriwa mkoani hapa.

" Ndugu mgeni rasimi sisi walimu hadi sasa tunaidai serikali zaidi ya shilingi bilioni 2 ambazo imekuwa ikiahidi kutulipa lakini mpaka sasa hakuna kwaiyo hali hiyo inapelekea sisi walimu kutokuwa na ile hali ya kuendelea kufundisha katika shule zetu hali ambyo inaweza kupelekea kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani hapa ".Alisema MASALU.

Nae mwenyekiti wa chama cha walimu mkoani hapa bwana HAMISI LISU amesema kuwa mbali na na walimu kuidai seriali fedha hizo hivyo atahakikishia kuwa kiwango cha elimu kinapanda mkoani hapa kwa kuwashawishi walimu kuwa wavumilivu wakati serikali ikiyatelekeza madai yao.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tabora AGREY MWANRI amesema kuwa ameyapokea madai hayo na kuwahakikishia walimu mkoani hapa kuwa atafuatilia kwa ukaribu madeni yote ili walim,u waweze kulipwa na kuendelea kufanya kazi kwa moyo mmoja bila kuwa na kinyongo chochote.

No comments: