Advertisements

Thursday, August 4, 2016

FREEMAN MBOWE AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI

Kiongozi wa Kambi rasmi  ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika wa Bunge amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe  akiagana  na Spika wa Bunge  Mhe. Job Ndugai alipomtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Bunge)

1 comment:

Anonymous said...

Kwanini tusiwe wakweli. Alikwenda uchunguzi wa afya ama kutibiwa? Si ni mgonjwa?