Advertisements

Monday, August 22, 2016

JESHI LA POLISI LAMKAMATA KIJANA AKIUZA FULANA ZA UKUTA

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limejiandaa kudhibiti maandamano ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta) yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu.
Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amewatoa hofu wakazi wa mkoa huo kuwa hakuna mtu na au kikundi chochote cha watu kitakachofanya maandamano siku hiyo.

“Habari ya Ukuta haipo,umeshabomoka na kama haujabomoka utabomoka, wakazi wa Dar es Salaam msiwe na hofu, fanyeni kazi na hata siku hiyo hakuna mtu atakayejitokeza barabarani kuandamana,” amesema.

Kamanda Sirro amedai kuwa siasa zinatakiwa kufanywa kwa amani na utulivu na kwamba wanasiasa wanaoitumia siasa kufanya vurugu hawatafanikiwa.

“Mimi niwahakikishie kwamba tunajiandaa kwelikweli kuhakikisha watu wanafuata sheria , anayetaka kuvunja sheria kwa kufanya maandamano aanze yeye ili nasi tuanze naye,” amesema.

Ameongeza kuwa ” Suala la utii wa sheria ni la msingi,kama kuna watu au kikundi cha watu kinataka kuitumia siasa kufanya uvunjifu wa amani wajue kwamba nafasi hiyo kwa Dar es Salaam haipo.”

Aidha,Kamanda Sirro amesema August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ ‘

  

Amesema  Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake

7 comments:

Anonymous said...

Wananchi wengi sana wanamuunga mkono Mhe Rais Magufuli. Mimi ningeshauri hawa wanademokrasia uchwara wa Chedema na wenzao waachwe kwa kupewa masharti. Pahala na muda. Wakikaidi washughulikiwe. Hata hao wafadhili wao itakuwa vigumu kuwaunga mkono katika ujinga huo. Hawa wasiitishe Serikali kiasi hicho. Wakifanya vurugu washughulikiwe vilivyo.

Anonymous said...

Udikteta kwakuwa walishindwa kura. Hawana ajenda hawa. Waiache Serikali ifanye yale iliyoahidi kwa wapiga kura wake na wananchi wake.

muungwana said...

Pamoja na Magufuli kuonyesha mwelekeo wenye matumaini kwa nini anakuwa na hofu sana na wapinzani? Yeye afanye kazi yake watu ndio wakaoamua mchele ni upi na chuya ni zipi! haiwezekani kufumba midomo watu wengine kwa kisingizio cha kuleta vurugu. kama nchi ni ya demokrasia kwanini wengine wafumbwe midomo! hao askari wanafanya nini, ndiyo wanaotakiwa kulinda maandamo kwani hao raia ni haki yao kikatiba! siyo kuwasambaratisha. Wana uhakika gani kwamba hayo maandamano yataleta vurugu, Polisi kazi yao ndiyo hiyo kuhakikisha hakuna atakayeleta vurugu wakati wa hayo maandamano,hawa polisi kazi yao siku zote ni kujikomba kwa watawala tu.Kama hataki mikutano ya siasa kwanini yeye Magufuli anakata mbuga kuwananga wapinzani wake, na yeye anatakiwa atulie afanye kazi zake siyo kutukana na kukebehi wenzake, msiwe wachovu wa kufikiri kiasi hicho! ukweli lazi
ma usemwe!

Anonymous said...

Kwani kufanya maandano ni uvunjaji wa sheria?nyie vipi acheni ushabiki maandazi.

Anonymous said...

Badala ya kukamata majambazi wanakamata tsheti

Anonymous said...

Nani kasema Magufuli anahofu na wapinzani. Tangu Tanzania iingie katika siasa ya vyama vingi hakuna hata uchaguzi mmoja uliofanyika na upinzani au wapinzani wakakubali matokeo kama wanavyofanya wenzetu wa ulaya na marekani, kila siku wameibiwa kura wao na kila mwaka baada ya uchaguzi wapinzani wanaandaa maandamano. Na kiundani haya maandamano ya ukuta sio kwa ajili ya demokrasia bali ni kumpinga muheshimiwa raisi sio raisi halali wa nchi aliechaguliwa kidemokrasia. Sasa utaona maandamano haya ya chadema ni kwa ajili ya kurejesha nyuma maendeleo ya demokrasia Tanzania. Kama chadema ni watu wa kuheshimu demokrasia basi wangetii amri ya raisi au wangeomba mwongozo moja kwa moja kutoka kwa raisi mwenyewe lakini waliloamua wao ni nguvu wanataka kushindana na serikali wanasahau yakuwa kushindana na serikali ni kushindana na wananchi waliowengi kwani ndio walioiweka madarakani serikali iliopo sasa. Maandamano yakifanyika katika nchi ambazo kiongozi akishindwa uchaguzi alafu anampigia simu mpinzani wake kumpongeza japo hata kama ilitokezea mizengwe katika uchaguzi huo kama vile tulivyoshuhudia marekani kati ya Bush na Gore au Bush John Kerry basi yanakuwa maandamano, lakini mpaka hii leo chadema na ukawa sijui upawa na Lowasa wao bado hawajakubali kushindwa na kukubali matokeo halafu hao watu uniambie wanaandaa maandamano ya kudai demokrasia lazima mtu mwenye akili timamu agune. Ni maandamano ya kudai demokrasia au ya kuchochea ughasi? Nafikiria Tanzania na watanzania wamechoka na amani kwani hata walibya waliaaminishwa yakuwa Ghadafi ni dikteta na akiondoka mambo yatakuwa mazuri zaidi na wapinzani Tanzania wanajaribu kuwaaminisha watanzania yakwamba demokrasia haipatikani isipokuwa kwa kuvurugu. Kama Nyerere Angeles kichwa chake kimeoza kama viongozi wengi wa upizani angeliwapotezea maisha watanzania wengi angewapeleka watanzania msituni kujiandaa kupambana na muengereza ndio Nyerere alikuwa na haki ya kufanya hivyo ni nchi yetu waengereza waliikalia kimabavu na kutufanya wageni ndani ya nchi yetu sasa kwa nini tusitumie nguvu kuikomboa. Lakini wazee walituambia nguvu huchuma cha jioni tu na ukiamka asubuhi ukatumwe tena lakini akili hutengeneza maisha. Sasa kama wapinzani wameamua kutumia nguvu kuionyesha serikali nani ana nguvu bismillah waache waanze. Na kama mimi ni Maghufuli kama raisi wa nchi hakuna haja ya kum,bembeleza mtu asiebembelezeka kwani walimzomea siku ya mwanzo kabisa alipokwenda kuwasalimu pale bungeni, alipolihutubia bunge kwa mara ya kwanza na hapo ndipo wapinzani walipo sibitisha ule usemi usemao, the first impression is the lasting impression. Hao watu hata Maghufuli afanye mazuri ya kiasi gani wataendelea kumpinga na kumrejesha nyuma vile vile kwa hivyo msimao mkali aliouchukuwa muheshimiwa raisi kukabiliana na watu ambao lengo lao kutaka kumuona anafeli,ni sahihi kabisa.

Unknown said...

Wakati wa kampeni kulikuwa na mikutano isiyopungua 15 kila siku na hakukuwa na fujo vyama vyote vilivyoweka wagombea udiwani vilifanya mikutano na maandamano bila fujo yoyote itakuwa chama kimoja peke yake?serikali tuepusheni na aibu hii,kutoa maoni kwa kutumia njia za amani ni haki ya kikatiba na kufanya mikutano kwa vyama vya siasa nihaki ya vyama vya siasa,waacheni wananchi na chadema watimize wajibu wao,kuupinga udikteta siyo kosa nchi yetu imefanya hivyo nara nyingi hadi nje ya mipaka yetu