Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamad, akisalimiana na viongozi wa chama hicho alipowasili Vuga mjini Zanzibar
kwa ajili ya Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi ambacho kilikuwa na Ajenda ya
tathmini ya mkutano mkuu maalum uliovunjika kutoka na vurugu. (Picha na Talib
Ussi).
Wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) wakiimba wimbo maalum wa
chama hicho ikiwa ni ishara ya kuaza kikao hicho chenye ajenda ya
tathmini ya mkutano mkuu maalum uliovunjika wiki iliyopita.
Na Talib Ussi, Zanzibar
Kikao cha Siku moja
cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF kimemalizika na kutoka na maamuzi mazito dhidi
ya viongozi na baadhi ya wanachama waliosababisha vurugu katika Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika wiki iliyopita.
Kikao hicho ambacho
kilifanyika huku jeshi la Polisi likizunguka katika maeneo mengi ya mji wa Zanzibar
kiliwashirikisha wajumbe wote kutoka Bara na Visiwani.
Katika kikao hicho kilichofanyika
Vuga katika ofisi za Chama hicho walikosekana wajumbe watatu ambao ni Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdelina
Sakay, Abdul Kambaya na Masoud ambao inadaiwa walionekana wazi katika kushabikia
vurugu ya mkutano wa wiki iliyopita.
Mapema
kikao hicho kilipangwa kufanyika katika Hotel Mansonz lakini kwa kile
kilichotwajwa hali uasalama ikaaamuliwa kifanyika ofisni hapo.
“Tumefanya maamuzi
magumu kuna wengine tayari tumewafukuza na wengine kuwasimamisha” kilisema
chanzo chetu kimaja kilichokataaa kutajwa jina lake.
Chanzo kilieleza kuwa
hali hakuwa rahisi lakini mwisho wa yoote walifikia maamuzi hayo kwa maslahi ya
chama ili kupeleka mapambano mbele katika kudai haki ya ushindi ya uchaguzi wa Zanzibar uluiofanyika October
mwaka jana.
Mkurugenzi wa habari wa chama hicho, Salim Biman alieleza kuwa hawezi kueleza chochote hadi Agosti 29 saa nne asubuhi ambapo watazungumza na waandishi wa habari ili kuweka hadharani
yale yote yaliopitishwa katika kikao hicho.
“Ninacho weza kukwambia
kesho tutaongea na waandishi ili tukupeni yoote lakini kwa sasa siko tayari
kueleza loloote naomba tukutane kesho” alieleza Biman.
Kikao hicho ambacho
kilifanywa katika hali ya tahadhari kilifuatiwa na kikao cha kamati Tendaji na
baadae Baraza Kuu.
No comments:
Post a Comment