Tundu Lissu akiwa mahakamani
Lissu ametimiza masharti ya dhamana baada ya mvutano mkali wa zaidi ya saa 5 na kujidhamini mwenyewe kwa dhamana ya shilingi milioni 10, na kesi yake imeahirishwa hadi Agost 19, 2016.
Mapema leo Katika Mahakama ya Hakimu MkazI Kisutu, ulinzi uliimalishwa tangu saa mbili asubuhi ambapo askari polisi waliokuwa na silaha walikuwa wakizunguka huku na huko kuhakikisha wafuasi wa chama hicho hawakusanyiki katika eneo la mahakama, huku kukiwa na matarajio ya kuwa wakati wowote atafikishwa mahakamani hapo.
Viongozi mbalimbali wa chama hicho nao walikuwepo katika mahakama hiyo kufuatilia kesi hiyo ya Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.
Majira ya saa tisa za alasiri Mhe Lissu alifikishwa mahakamani na kupandishwa kizimbani.
Akisomewa Mashataka na Wakili wa Serikali Paul Kaduche mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkahe imeelezwa kuwa Mhe Tundu Lissu alifanya makosa hayo matatu Agost 2 mwaka huu, katika maeneo ya mahakama hiyo, kwa kutoa maneno ya uchochezi, maeneno ya dharau katika mfumo wa utoaji haki pamoja na kuidharau mahakama ya Kisutu.
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na baadaye ukatokea mvutano wa kisheria juu ya uhalali wa dhama ambapo mawakili wa serikali walikuwa wakipinga mtuhumiwa huyo kupewa dhamana.
Baada ya mvutano wa zaidi ya saa 5, kuanzia saa 10 jioni hadi saa 2:50 usiku, ambapo hakimu alikubali hoja za upande wa utetezi na kutoa dhamana baada ya Lissu kukamilisha masharti ya dhamana hiyo.
Mara baada ya kuchiwa, Lissu akiongozana na baadhi ya viongozi wa chama chake, aliondoka mara moja mahakamani hapo.
3 comments:
..Katika nchi za Kiafrika, mara zote uhasama ambao huzaa vita vy wenyewe kwa wenyewe huletwa na Viongozi ambao hujiona kama Miungu...yaani wao wapo kamili( Perfect) Hawataki kukosolewa....
Kwa haya ya Tundu Lissu ni Aibu ya Taifa....
Leo hii Taifa la Baba Nyerere linaweza kumfanyia mbunge mambo hayo.???
..Tunajiingiza kwenye Aibu ya Kimataifa bila jambo la msingi...
Usiandike usichokiamini.Hivi unadhani Nyerere angestahimili kumuona mbunge anaechochea uvunjifu wa amani au kumtokea kashfa? Ni Nyerere yupi unaemuongelea wewe?
Ni hawa hawa Ukawa ambao wakipewa platforms za kutetea uhuru zaidi kupitia mabadiliko ya katiba au bunge wanaishia kususia kwa sababu zisizokuwa na mashiko.Leo hii wanataka ku - mobilize vurugu kwa yalex2 waliyosusia awali! Pathetic
Wenzetu vioja hivi ndio kula yao. Kikwete alisema, Akili ya Mwenzako ongeza na yakwako!
Post a Comment