Advertisements

Monday, August 22, 2016

MBWANA SAMATTA AENDELEA KUTIKISA NYAVU UBELGIJI

Mbwana Samatta ameendelea kuwasha moto kwenye ligi ya Ubelgiji (Jupier Pro League) baada ya kufunga magoli mawili kwenye ushindi walioupata ugenini KRC Genk wa magoli 3-0 dhidi ya KSC Lokeren.

Magoli ya Genk yalifanikiwa kufungwa na Samatta kwenye dakika ya 34 na 38 na baadaye dakika ya 48 Leon Bailey alihitimisha ushindi wa mabao matatu ulioipa pointi tatu timu hiyo.
Samatta ameonekana kuanza msimu vizuri baada ya kufanikiwa kufunga magoli mawili kwenye mechi za Europa kwenye hatua ya kuwania nafasi ya mtoano na kuingia kwenye hatua ya kati ya mechi tatu walizocheza.
Tazama magoli yote hapa.

No comments: