Advertisements

Sunday, August 28, 2016

Meya Ilala azuia wamachinga kuondolewa katikati ya jiji

Meya wa Ilala, Charles Kuyeko akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar. Picha na Salim Shao

By Suzan Mwillo, Mwananchi


Dar es Salaam. Meya wa Ilala, Charles Kuyeko amesema wamachinga waendelee kufanya biashara mjini na wasibughudhiwe na mtu yoyote.

Kauli ya Kuyeko imekuja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene kuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa machinga maeneo ya katikati ya jiji.

Hivi karibuni alipokuwa Mwanza, Rais John Magufuli aliruhusu wafanyabiashara hao waendelee kufanya kazi kati kati ya mji hivyo hata wa jijini hapa wanaguswa na kauli hiyo.

2 comments:

Anonymous said...

Waziri wa TAMISEMI ana mamlaka zaidi yako wewe meya wa Ilala. Ungekuwa msomi ungeielewa vizuri hotuba ya Rais kuhusu wamachinga. Huko Mwanza hawajawekewa sehemu maalumu ya kufanyia biashara na ndiyo Rais akaamuru waendelee na biashara zao mjini mpaka hapo watakapopatiwa sehemu muafaka. Msipende kupotosha wananchi na kusababisha ghasia zisizokuwa na maana

Anonymous said...

Tusitegemee kupata maendeleo kwa mwendo huu.Acheni kutafuta political milage kwenye nafasi zakiutendaji.
Mayor anapaswa kufahamu kuwa yeye ni mayor wa Dar es Salaam na sio wa Mwanza au wa Tanzania. Hivyo anapaswa kusimamamia kuondoa kero na kuleta maendeleo Dar.Yaliyoamuliwa Mwanza hayamuhusu.