Advertisements

Tuesday, August 2, 2016

MREMA AMTAKA LOWASSA AKUBALI KWAMBA ALISHINDWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA JANAMwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati)akisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao  jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenekiti wa Waendesha Bodaboda na Bajaj wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede na kushoto ni Katibu wake Bw. George Mbwale.


Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ambaye pia ni Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amemtaka Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akubali kwamba alishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na akae kimya hadi mwaka 2020.

Mrema aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam na kusisitiza kwamba alimtaka Waziri Mkuu Mstaafu watoke CCM pamoja kwa kuwa nguvu ya upinzani ilikuwa kubwa sana.

‘’Mimi nitamuuliza 1995 wakati natoka nilikuambia tutoke sasa maji yamechemka tukiweka unga tutakula ugali ukagoma, ukasema unaendelea kula kidogo hadi alipojiuzulu akaendelea na CCM hadi alipotaka kugombea Urais akakataliwa na wenzake ndipo akaja upinzani’’

Mrema aliongeza kwamba Chama cha Mapinduzi kilitakiwa kuondoka madarakani mwaka 1995 ambapo yeye ndiye alikuwa na nguvu kubwa ya kisiasa nchini.

Aidha Mrema amewataka vijana kuwa makini na upinzania kwa kuwa Lowassa alijiunga na upinzani baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea Urais ndani ya CCM hivyo wajiepushe na maandamano kwani hayana faida kwao.

1 comment:

Anonymous said...

Hakika kabisa hakuna kitu kilichompeleka Lowasa upizani kama si uroho wa madaraka. Kwa maana yakwamba kama Lowasa angepitishwa kugombea uraisi kwa ticket ya CCM asingetoka. Na mbaya zaidi amekwenda kuhamia chama ambacho kina harufu ya ukanda kwa mtazamo wowote ule. Siasa za kiafrika kwa kiasi kikubwa ni balaa tu bado tuna safari ndefu.